October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Muuguzi ajitosa ubunge Singida

Ukende William Shalla akikabidhiwa fomu ya kugombea ubunge viti maalum kupitia Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Singida na Katibu wa umoja huo mkoani humo, Edina Kugulu.

Spread the love

UKENDE William Shalla, amechukua na kurejesha fomu ya kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kugombea ubunge Viti Maalum mkoani Singida. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Shalla ambaye ni mtaalamu wa tiba ya uuguzi na ukunga, amerejesha fomu hiyo jana Jumatano tarehe 15 Julai 2020, katika Ofisi za CCM mkoa wa Singida, ambapo ilipokelewa na Edina Kugulu, Katibu wa Umoja wa Wanawate Tanzania (UWT), mkoani Singida

Mwanasiasa huyo alichukua fomu hiyo tarehe 14 Julai 2020, ambapo ametia nia kugombea ubunge Viti Maalum kupitia kundi la wanawake.

Akizungumza baada ya kurejesha fomu hiyo, Shalla alisema, ameamua kugombea nafasi hiyo ili akawawakilishe wanawake bungemi, ikiwemo kueleza changamoto zao.

CCM ilifungua zoezi la uchukuaji na urejeshaji fomu za kugombea nafasi ya ubunge, uwakilishi, udiwani na nafasi za viti maalum, tarehe 14 Julai 2020.

Kwa mujibu wa ratiba ya CCM, zoezi hilo linatarajiwa kufungwa kesho Ijumaa tarehe 17 Julai 2020.

error: Content is protected !!