April 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Muuaji New Zealand kukumbwa na hukumu ya kihistoria

Spread the love

MTUHUMIWA wa mauaji ya watu 50 katika misikiti miwili iliyoko mjini Christchurch, New Zealand, Brenton Tarrant (28) huenda akakumbwa na adhabu ya kihistoria. Inaripoti mitandao ya kimataifa … (endelea).

Terrant aliyeshtakiwa kwenye Mahakama ya Wilaya ya Christchurch kwa makosa 50 ya mauaji pamoja na makosa 39 ya kutaka kufanya majaribio ya mauaji katika misikiti hiyo, anatarajiwa kuwa mfungwa wa kwanza wa kifungo cha maisha jela pasipo kuwa na uwezekano wa kupewa msamaha kama ilivyo desturi ya taifa hilo.

Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa, leo Alhamisi tarehe 4 Aprili 2019 ameongezewa mashtaka kadhaa, hali inayoashiria kwamba, mtuhumiwa huyo atakuwa wa kwanza kupewa adhabu ya kifungo cha maisha jela pasipo na uwezekano wa kupewa msamaha.

Kwa sasa Tarrant amewekwa rumande katika gereza lililoko mjini Auckland hadi pale kesi yake itakapopangiwa tarehe ya kutajwa na mahakama ya Christchurch, kwa ajili ya kusikilizwa.

Tarrant anadaiwa kufanya shambulizi la mauaji la risasi katika miskiti ya Al-Noor na Lin Wood wiki tatu zilizopita, na kusababisha vifo vya watu 50 na majeruhi 39.

error: Content is protected !!