Wednesday , 27 September 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa ‘Muuaji msikitini New Zealand alijaza silaha kwenye gari lake’
Kimataifa

‘Muuaji msikitini New Zealand alijaza silaha kwenye gari lake’

Spread the love

BRENTON Tarrant (28) aliyeshiriki kufanya mauaji msikitini nchini New Zealand jana tarehe 15 Machi 2019 na kusababisha vifo vya waumini wa dini ya kiislam 49, amekutwa na silaha nyingi kwenye gari alilotumia. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Uchunguzi wa awali uliofanywa na Jeshi la Polisi nchini humo umeeleza kuwa, Tarrant ambaye ni raia wa Australia ameshiriki kwenye mauaji hayo ya kikatili katika Mji wa Christchurch tayari amefikishwa mahakamani.

Jacinda Arden, Waziri Mkuu wa New Zealand akizungumza na vyombo vya habari leo tarehe 16 Machi 2019 amesema, uchunguzi wa awali unaonesha kwamba, Tarrant alitoka na bunduki tano kwenye gari hilo.

Amesema, bunduki zilizotumiwa na mtuhumiwa katika kutekeleza shambulio hilo zilikuwa zimebadilishwa ambapo gari lake alikuwa amelijaza silaha pamoja na leseni za silaha.

Tarrant ameendelea kuwekwa kizuizini baada ya kunyimwa dhamana na kwa mara nyingine anatarajiwa kupandishwa kizimbani tarehe 5 Aprili mwaka huu.

Wakati Tarrant akifunguliwa shitaka la peke yake la mauaji, watuhumiwa wengine watatu akiwemo mwanamke mmoja na wanaume wawili wanaendelea kuwekwa kizuini na Jeshi la Polisi nchini humo.

Waziri Arden amesema, serikali ya New Zealand itatoa msaada wa kifedha kwa familia zilizopoteza ndugu zao katika tukio hilo.

Meya wa Mji wa Christchurch ambako kulitokea tukio hilo jana alfajiri, Lianne Dalziel amesema bendera zilizoko katika majengo ya serikali zitasimamishwa nusu mlingoti hadi pale taarifa zaidi zitakapotolewa.

Tukio hilo la kusikitishalililopoteza maisha ya watu 49 na kuacha majeruhi 48, lilitokea katika misikiti miwili- Lin Wood na Al Noor.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Mahakama yamkuta na hatia Donald Trump

Spread the love  ALIYEKUWA Rais wa Marekani, Donald Trump, amekutwa na hatia...

Kimataifa

Harusi yageuka msiba 100 wakifariki kwa ajali ya moto

Spread the love  WATU takribani 100, akiwemo bibi na bwana harusi, wamefariki...

Kimataifa

Kampuni ya mali ya China Oceanwide yapata agizo la kufilisiwa huko Bermuda

Spread the love  MAHAKAMA ya Bermuda imetoa amri ya kufilisiwa kwa Kamapuni...

Kimataifa

Uvamizi wa kijeshi Milango ya bahari ya Taiwan G7 yapinga China

Spread the loveMKUTANO wa Mawaziri wa Mambo ya nje wa nchi za...

error: Content is protected !!