June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mutungirehi aitosa TLP, ahamia Chadema

Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP), Augustine Mrema

Spread the love

MBUNGE wa zamani wa Jimbo la Kyerwa mkoani Kagera 2000-2005, Benedicto Mutungirehi, amekihama Chama chake cha Tanzania Labour (TLP) na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Anaandika Mwandishi wetu … (endelea).

Mutungirehi ambaye ni mwanasiasa msomi, amefikia uamuzi huo jana jimboni Kyerwa na kutangaza nia yake ya kuwania ubunge katika uchaguzi mkuu ujao Oktoba mwaka huu.

Akiongozana na wanachama wenzake 26 wa TLP, Mutungirehi alikabidhiwa kadi ya Chadema na mwenyekiti wa chama hicho wilayani Kyerwa, Deus Rutakyamirwa.

Katika uchaguzi mkuu wa 2000, Mutungirehi alishinda kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) lakini akaenguliwa kwenye vikao vya uteuzi, jambo lililowafanya wananchi wa Kyerwa kumlazimisha ahamie upinzani.

Baada ya kutii sharti hilo, wananchi walimchagua kwa kura nyingi kuwa mbunge wao na hivyo kumshinda aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Justuce Katagira.

Hata hivyo, katika uchaguzi mkuu uliofuata mwaka 2005, Mutungirehi aliangushwa na Katagira ambaye analishikilia jimbo hilo hadi sasa kutokana na TLP kupoteza mvuto baada ya mwenyekiti wake, Augustine Mrema kuporomoka kisiasa.

Zimekuwepo juhudi za muda mrefu sasa za wananchi wa Kyerwa kumshawishi Mutungirehi ahamie Chadema na kugombea ubunge kutokana na chama hicho kujijengea mtandao mkubwa ambao unampa uhakika wa kushinda.
Mutungirehi alirejea rasmi katika siasa za jimbo la Kyerwa wakati wa kufunga kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa ambapo alikuwa mgeni rasmi kakika mkutano Ukawa uliofanyika Nkwenda stand na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi.

error: Content is protected !!