January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Muslim kumng’oa Zungu Ilala

Mbunge wa Ilala, Musa Zungu ambaye amepata mpinzani kutoka Chadema

Spread the love

MJUMBE wa Bodi ya Wadhamini katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Muslim Haiderally Hassanali (32), amerejesha fomu na kutangaza nia yake ya kumng’oa Mbunge wa Ilala, Azani Zungu, katika Jimbo la Ilala. Anaandika Pendo Omary … (endelea).

Muslim amekabidhi fomu hiyo kwa Casimir Juma Mabina, mratibu wa chama hicho, Kanda ya Pwani.

Akizungumza baada ya kukabidhi fomu zake, Muslim amesema, “Nimeamua kugombea jimbo la Ilala kwa sababu, kwa zaidi ya miaka 10 sasa, limeshindwa kupata mwakilishi sahihi.” 

Amesema,  “Kama kupigika watu ni Dar es Salaam jimbo la Ilala. Kama ni kuwakimbiza watu ni Dar es Salaam jimbo la Ilala. Kama ni shida za foleni zinaanzia jimbo la Ilala, kama ni shida za afya ni Ilala. Nimekulia Ilala, nimesomea Ilala na naifahamu vizuri Ilala ndio maana nagombea Ilala,” ameeleza Muslim.

Aidha, Muslim amesema anafahamu kuna utaratibu wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa). Lakini ameona atangaze nia kupitia chama chake cha Chadema na indapo maamuzi ya Ukawa hayatampitisha kuwania jimbo hilo atakuwa tayari kuheshimu maamuzi hayo na kumuunga mkono mgombe atakayeteuliwa.

“Enzi za kuibudu, kuigopa CCM imeisha, Nitafarijika Ukawa ikinipitisha. Watu wangu wa Ilala waniunge mkono. Zungu ameiongoza Ilala kwa miaka 10, kwa jinsi alivyoongoza watu wanajua, kama ameshidwa kuwatetea wanajua. Hivyo watupishe sisi chadema ili tulete maendeleo….

“Hatuwezi kutegemea CCM kuwa na wapiganaji bora kuliko chadema na Ukawa . CCM ni taasisi ambayo imejaa vituko ndani yake. Kuna kila uozo kama ni rushwa wanaongoza ni wao. Wamejitokeza zaidi ya watu 35 kugombea nafasi ya urasi. Ni watu wa kambi fulani wanafanya maigizo,” amesisitiza Muslim.

Naye Mwenyekiti wa kanda hiyo na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chadema Mabere Marando amesema “Sisi tunaamini katika jimbo la Ilala tuna mgombea bora. ndio maana mimi kama Mwenyekiti wa kanda hii nimemuomba na kumhimiza ndugu  yangu Muslim ajitokeze kugombea. Tunaamini kabisa wenzetu wa ukawa watatuunga mkono tutapata ushindi.”

Muslim alizaliwa 29 Septemba 1983. Alijiunga rasmi na Chadema mwaka 2002. Ameo mke mmoja. Aliwahi kugombea jimbo la Kigoma Kusini na kuweka rekodi ya kuwa mgombea mdogo katika Uchaguzi mkuu mwaka 2005.

Mbali na Muslim, Wanachama wengine wa chama hicho Raphael Machinda (kata ya Mchikichini) naMashiku Chokola (kata ya Kivukoni) wamerejesha fomu wakiwania udiwani katika kata hizo.

error: Content is protected !!