Sunday , 19 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Museveni kung’oka madarakani?
KimataifaTangulizi

Museveni kung’oka madarakani?

Spread the love

RAIS wa Jamhuri ya Uganda, Yoweri Kaguta Museveni, aweza kung’oka madarakani ndani ya kipindi cha miaka miwili kutoka sasa. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea). 

Taarifa kutoka nchini Uganda zinasema, shinikizo la kutaka Museveni aachie madaraka, mbali ya kupamba moto ndani ya nchi yake, limeanza pia kupata msukomo kutoka jumuiya ya kimataifa. 

“Huyu Museveni hawezi kumaliza hata miaka miwili kabla ya kung’atuka madarakani, iwe kwa hiari au kwa shinikizo. Hii ni kwa kuwa tayari wananchi wengi wameanza kumchoka na Jumuiya ya Kimataifa, inamhusisha na kinachoendelea kule Sudan ya Kusini,” anaeleza raia mmoja wa Uganda.

Akihojiwa na televisheni ya KNT ya Kenya, raia huyo ambaye ni mchambuzi wa masuala ya kisiasa alisema, “hakuna njia nyingine ya Museveni kuendelea kubaki madarakani kwa miaka mingine 10 ijayo. Anachoweza kufanya ni kuondoka mwenyewe kwa hiari, ama kusubiri umma umuondoe.”

Kupatikana kwa taarifa hizi kumekuja katika kipindi ambacho upinzani unaongozwa na mbunge wa Kyadondo, Robert Kyagulanyi Ssemtamu (Bobi Wine), ukimshinikiza Museveni kuondoka madarakani.

Aidha, kupatikana kwa taarifa hizi kumekuja wakati raia wa Uganda walioko nje wakiendelea kuishtumu serikali yake kwa kile wanachokiita, “vitendo vya unyanyasaji  kwa wanasiasa wa upinzani na raia wa kawaida.”

Katika mji wa Toronto nchini Canada, kumeibuka maandamano makubwa kwenye barabara za mji huo kumshutumu Museveni, huku raia wengine waishio Marekani na Afrika Kusini, wakituma kanda za video kulaani serikali yao.

Yoweri Kaguta Museveni, ni rais wa 29 wa Uganda. Aliingia madarakani Januari 1986, baada ya kushinda vita vya msituni chini ya kundi la National Resistance Movement (NRM). Akatangazwa kushinda uchaguzi wa urais wa mwaka 1996, 2001 na 2006. Amezaliwa katika wilaya ya Ntungamo.

Kabla ya kuwa rais wa taifa hilo, Museveni aliongoza mapambano dhidi ya serikali za Idd Amin aliyetawala kati ya mwaka 1971 na 1979 na Milton Obote aliyeshika madaraka kati ya mwaka 1980 hadi 85.

Kutokana na mafanikio yake katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi na kuridhia sera za Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha Duniani (IMF), Museveni alipata sifa kubwa toka kwa viongozi wa mataifa ya Magharibi.

Mwishoni mwa miaka ya 1990, alikuwa akielezewa kuwa ni mfano bora wa kizazi kipya cha viongozi wa Afrika.

Hata hivyo, uongozi wake umetiwa dosari na mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na ushiriki wake katika vita vya wenyewe kwa wenyewe katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Rwanda. Anatuhumiwa pia kushiriki katika vita vinavyoendelea Sudan Kusini.

Analaumiwa kwa ukiukwaji wa haki za kisiasa na zile za kibinadamu unaofanywa na serikali yake dhidi ya wapinzani kama vile Kizza Besigye na kitendo cha kubadili katiba ya nchi hiyo ili aweze kugombea urais mwaka 2006.

Wiki tatu zilizopita, vyombo vya usalama vilimkamata na kumuweka kizuizini, Bob Wine, jambo ambalo lilimfanya Museni kutoka hadharani kueleza aliko mbunge huyo na afya yake kwa ujumla.

Hii ni baada ya kuwepo tishio la kufanyika kwa maandamano makubwa nchi mzima ya kumpinga.

Katika taarifa yake ya kwanza kwa umma kuhusu afya ya mbunge huyo, Museveni amevishutumu vyombo vya habari kwa kile alichokitaja ni kueneza habari zisizo za kweli kuhusu suala hilo.

Kulingana na ripoti mbalimbali za vyombo vya habari mbunge huyo ambaye pia ni msanii, alidaiwa kuwa na matatizo ya figo ambayo yanahitaji kutibiwa ipasavyo na madaktari bingwa na waliobobea katika kutiba sehemu nyeti kama hizo za ndani ya mwili.

Rais Museveni alilaumu aliowaita, “watu maalum” ambao alieleza kuwa ni wa kutoka nje wanaotafuta kuingilia siasa za nchi hiyo.

Alisema, “…vyombo vya kueneza habari zisizo za kweli vimekuwa vikitangaza kwamba mjukuu wetu, asiye na nidhamu Bobi Wine, ni mgonjwa mahututi, hawezi kuzungumza na mengineyo.

“Wamekuwa wakisema kuwa huenda maafisa wa usalama wamemjeruhi vibaya Bobi Wine kwasababu ya namna walivyokabiliana na wabunge wakati wakiwakamata.

“Nimeamua kuwasiliana na madaktari wa jeshi, kwasababu ya nidhamu ya jeshi, madaktari wa UPDF daima wanachukua tahadhari katika hali kama hizi. Tayari Bobi Wine alionekana na madaktari Arua, Gulu na Kampala. Hakuwa na majeraha ya kichwa, kifua au mifupa kuvunjika, wameniarifu.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Lissu akabidhiwa gari lake, aomba msaada wa matengenezo

Spread the loveMakamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu leo Ijumaa amekabidhiwa...

Habari za SiasaTangulizi

Haya hapa majina walioteuliwa kugombea nafasi mbalimbali CHADEMA

Spread the loveCHAGUZI wa kanda za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Uingereza yamwaga bil. 9 kumuunga mkono Samia matumizi nishati

Spread the loveWaziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Selemani...

error: Content is protected !!