Friday , 3 February 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Museveni ampinga Askofu kuwazuia wasichana wajawazito kurudi shuleni
Kimataifa

Museveni ampinga Askofu kuwazuia wasichana wajawazito kurudi shuleni

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni
Spread the love

 

RAIS wa Uganda, Yoweri Museveni amepinga uamuzi wa Askofu wa Kanisa la Uganda la kuwazuia wasichana wajawazito kurudi shuleni baada ya shule kufunguliwa mwezi huu nchini humo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Hatua hiyo imekuja baada janga la maambukizi ya Covid- 19 ambapo shule zilifungwa nchini humo kwa kipindi cha miaka miwili huku wasichana wengi wakipata ujauzito.

Askofu wa Kanisa la Uganda Dayosisi ya Mukono, James Ssebgala aliwaamuru walimu wa shule zinazomilikiwa na Kanisa la Uganda zisiwaruhusu wanafunzi wajawazito kurudi shule baada ya kufunguliwa nchini Uganda tarehe 10, Januari mwaka huu.

Askofu huyo alipinga mpango wa wizara ya elimu nchini Uganda wa kuwaruhusu wanafunzi wote waliopata ujauzito na wale waliojifungua wakati wa zuio la kukaa nyumbani karibu miaka miwili warudi shuleni kuendelea na masomo.

Aliwataka walimu kuwapeleka wanafunzi katika vituo vya afya wapimwe kabla ya kuanza masomo na atakayepatikana na ujauzito wamrudishe nyumbani.

Museveni alipinga agizo hilo wakati akihutubia wananchi katika maadhimisho ya miaka 36 ya chama chake cha NRM kuingia madarakani.

“Kitu ambacho naweza kuwaambia wazi kwamba sikubaliani nacho, ni kuzuia msichana asiendelee na masomo kwa sababu alipata ujauzito kwa mara ya kwanza, siwezi kukubalina na hilo.

“Hata katika masuala ya kidini… kwa sababu mtoto kama alifanya makosa huwezi kumlaani katika maisha yake yote na kumkatisha masomo yake.

“Mbona kuna mama wazee zaidi ya miaka 50 wanarudi shuleni kusoma? kwanini umkatize mtoto masomo wakati alipata matatizo?.Alihoji Rais Museveni.

Tangu shule zifunguliwe nchini Uganda tarehe 10 mwezi huu kulingana na takwimu za wizara ya elimu, kati ya wanafunzi milioni 15 nchini humo kabla ya zuio la janga la corona aslilimia 30 hawajarudi shuleni huku wengine sababu ikiwa ni ujauzito na kujifungua na wengine wazazi kushindwa kulipa karo za shule.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Hospitali za China zilifurika wagonjwa, wazee kipindi cha wa likizo ya Mwaka Mpya wa Lunar

Spread the loveHOSPITALI  nchini China zimejaa wagonjwa na wazee katika kipindi cha...

Kimataifa

Papa Francis ayataka mataifa ya nje kuacha kupora mali DRC

Spread the love  KIONGOZI wa kanisa Katoliki Papa Francis, ameyataka mataifa ya...

Kimataifa

Mashabiki wakabiliwa na mashtaka ya mauaji baada ya wafuasi wa Arsenal na Manchester City kupigana Uganda

Spread the love  MASHABIKI wawili wa soka nchini Uganda wanakabiliwa na mashtaka...

Kimataifa

China inatathmini upya sera za wafanyakazi

Spread the love  WAKATI idadi ya watu wa nchi China inapungua, Beijing...

error: Content is protected !!