RAIS wa Uganda, Yoweri Museveni, ametangaza barabara lake jipya la mawaziri, lenye mawaziri 32, akiwemo mke wake, Janet Museveni, aliyemteuwa kuwa Waziri wa Elimu nchini humo. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).
Rais Museveni ametangaza baraza hilo usiku wa jana, tarehe 8 Juni 2021, wiki kadhaa baada ya kuapishwa kuendelea na muhula wake wa sita, wa uongozi wa Taifa hilo, tarehe 12 Mei mwaka huu.
Katika safu hiyo ya mawaziri, Rais Museveni ameteua manaibu waziri 50 na kufanya idadi ya mawaziri nchini humo kuwa 82.
Mbali na uteuzi wa baraza la mawaziri, Rais Museveni amemteua Meja Mstaafu wa Jeshi, Jessica Alupo, kuwa Makamu wake wa Rais, wakati aliyekuwa Waziri wa Afya, Robinah Nabanja, akimteua kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo.
Rais Museveni amechukua hatua hiyo, baada ya kushinda kiti cha Urais wa Uganda, katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 14 Januari 2021, akichuana vikali na aliyekuwa Mbunge wa Kyadondo, Robert Kyagulanyi, maarufu kama Bobi Wine.
Rais Museveni ameiongoza Uganda kuanzia tarehe 29 Januari 1986, alipompindua aliyekuwa Rais wa Taifa hilo, Milton Obote.
Leave a comment