Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Museveni ajiimarisha Ikulu, amteua mwanaye kumlinda
Habari za Siasa

Museveni ajiimarisha Ikulu, amteua mwanaye kumlinda

Yoweri Museveni
Spread the love

RAIS wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni, amemteuwa mwanaye Luteni Jenerali Muhoozi Kainerugaba. kuwa mkuu wa kikosi cha ulinzi wa Rais (SFC). Inaripoti mitandao ya kimataifa…(endelea).

Jenerali Muhoozi, ni mtoto wa kwanza wa rais huyo ambaye amekuwa madarakani kwa miongo minne sasa. Kabla ya uteuzi huo, Jenerali Muhoozi, alikuwa mshauri wa baba yake – Rais Museveni – katika masuala ya ulinzi.

Kabla ya kuteuliwa tena kwenye wadhifa wa mshauri wa rais wa masuala ya ulinzi, Jenerali Muhoozi aliwahi kushika cheo huko nyuma.

Rais Museveni ambaye ni amiri jeshi mkuu wa Uganda, ameamua kumrejesha mwanaye kwenye nafasi hiyo baada ya kufanya mabadiliko kuelekea kipindi hicho cha uchaguzi mkuu wa rais, unaotarajiwa kufanyika Januari mwakani.

Mabadiliko hayo yamefanyika katika kipindi ambacho taifa hilo la Afrika Mashariki, linatuhumiwa na mataifa ya Magharibi na Ulaya, kwa ukiukwaji wa haki za binadamu.

Aidha, baadhi ya wanasiasa wa upinzani nchini humo, wanamnyooshea kidole Museveni na serikali yake, wakiwatuhumu kwa mateso dhidi ya raia, kuvuruga mikutano ya kisiasa, kuwakamata na kuwafunga.

Katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu, Uganda imekuwa ikabiliwa na maandamano kutoka kwa wananchi wake, wanaopinga utawala wa Museveni, ambao umeingiza nchi kwenye machafuko na ugumu wa maisha.

Katika uchaguzi huu, Rais Museveni anakabiliwa na kibarua kigumu kutoka kwa Bobi Wine.

Mwanasiasa huyo machachari nchini Uganda, anaonekana kuungwa mkono, hasa na kizazi chenye njaa na hasira; ambacho kimeamua kupigania uhuru wa taifa hilo.

Wiki tatu zilizopita, maelfu ya vijana nchini Uganda, walifanya maandamano na ghasia kupinga kukamatwa kwa Bob Wine, ambapo watu zaidi ya 28 wakiripotiwa kufariki dunia

Bobi Wine

Akiwahutubia wafuasi na maafisa wa chama chake cha People’s Power, mjini Kampala, Bobi Wine alisisitaiza, damu ya raia wasiokuwa na hatia iliyomwagika haitaenda bure, na kuongeza kuwa “haki itatekelezwa.”

Mgombea huyo wa urais amesema, mashambulio yaliyofanywa dhidi ya raia, yameweka wazi udhalimu wa serikali inayoongozwa na Museveni.

Njia ya Museveni ya kutakiwa kustaafishwa kwa lazima, ilianza mshindani wake huyo, aliposhinda uchaguzi mdogo wa ubunge katika wilaya ya Kyadondo Mashariki, Uganda ya Kati.

Bob Wine ambaye aligombea kama mgombea binafsi, aliwashinda wagombea kutoka chama tawala, National Resistance Movement (NRM) na kile cha upinzani, Democratic Change (FDC).

Mara baada ya kutangazwa kwa mshindi katika uchaguzi huo, Bob Wine aliahidi kuwaunganisha raia wote wa Uganda kwa kusema, “ninataka kufanikisha maridhiano. Ninataka siasa zitulete pamoja.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!