August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Museveni abadili uongozi wa jeshi

David Muhoozi (katikati)

Spread the love

YOWERI Museveni, Rais wa Uganda amefanya mabadiliko katika jeshi la nchi hiyo kwa kumteua David Muhoozi kushika nafasi ya Mkuu wa Majeshi (CDF), anaandika Wolfram Mwalongo.

Awali, nafasi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na Edward Katumba Wamala ambapo sasa ameteuliwa kuwa Waziri wa Kazi nchini Uganda.

Kabla ya Muhoozi kuteuliwa katika nafasi ya CDF, alikuwa kiongozi mkuu wa jeshi la ardhi la nchi hiyo.

Katika mabadiliko hayo, Rais Museveni amemteua mtoto wake Muhoozi Kainerugaba kuwa mshauri mwandamizi wa masuala ya oparesheni maalum. Kabla ya mtoto huyo kutwaa nafasi hiyo, alikuwa mkuu wa kikosi maalumu (SDF).

SDF ni kitengo cha juu kinachomshauri rais hususani katika masuala ya kiulinzi pamoja na mambo nyeti ya taifa.

Aidha, amemteua Wilson Mbadi, aliyekuwa Mkuu wa Utumishi na Mlinzi wa rais huyo (bodyguard) kwa muda mrefu kuwa msaidizi wa CDF.

error: Content is protected !!