Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Muro wa NCCR-Mageuzi aahidi kuibadili Kinondoni
Habari za Siasa

Muro wa NCCR-Mageuzi aahidi kuibadili Kinondoni

Spread the love

MUSTAFA Muro, Mgombea Ubunge wa Kinondoni jijini Dar es Salaam kupitia NCCR-Mageuzi, ameahidi kuboresha maisha ya wananchi wa jimbo hilo, endapo watamchagua katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Pia, ameahidi kuwawesha wananchi kiuchumi kwa kuhakikisha wanapata mitaji na elimu ya biashara.

Muro ametoa ahadi hizo leo Alhamisi tarehe 10 Septemba 2020 katika uzinduzi wa kampeni zake Kata ya Mdugumbi-Magombeni. Uzinduzi huo umefanyaa na James Mbatia, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi.

Amesema, akifanikiwa kuwa mbunge atahakikisha fedha za mikopo zinatolewa na Halmshauri zinawafikia walengwa bila ubaguzi, pamoja na kuwapatia watalaamu wa biashara na uchumi wananchi wanaofanya biashara ndogondogo ili wakuze mitani yao na kujikwamua kiuchumi.

“Kuna haki mbalimbali ya mikopo, mimi wakati nikiwa Diwani Kinondoni niliwapa mikopo watu wa aina zote, kuna watu walisema usiwape wale lakini sikuwasikiliza kwa kuwa unapokuwa kiongozi wa watu, unatakiwa¬† utumikie wote na uwe na uongozi shirikishi,” amesema Muro.

Muro alikuwa Diwani wa Kinondoni kupitia Chadema mwaka 2015-2020 kisha baada ya kunaliza muda wake akahamia NCCR-Mageuzi.

Wakati huo huo, Muro amesema akiwa mbunge, atahakikisha wananchi wake wanapata huduma bora za afya, hasa wazee ambao watapewa huduma hiyo bure kwa mujibu wa sera na sheria za nchi.

Pia, atahakikisha wanapata huduma ya maji safi na elimu.

Muro ameahidi kutatua changamoto za miundombinu ya barabara, mitaro ya kusafirishia maji taka na uchafu wa mazingira.

“Kinondoni kuna changamoto ya mitaro kuziba, nikiwa mbunge nitahakikisha naipanua mitaro, pamoja na kuboresha miundombinu ya barabara za mitaa. Pia, nitahakikisha taka zinazolewa kila mara ili kuondokana na mrundikano wa takataka,” amesema Muro.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

M/kiti bodi ya wadhamini Chadema afariki dunia

Spread the loveMWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na...

Habari za Siasa

Zitto: Nikifa Ado atavaa viatu vyangu

Spread the love  KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe...

error: Content is protected !!