January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Muonekano wa Iphone 6 ni babu kubwa

Iphone 6

Spread the love

Hata hivyo Samsung Galaxy Note 4 bado kinara

Samsung Galaxy Note 4
Samsung Galaxy Note 4

iPhone 6 na iPhone 6 Plus ni simu za kisasa zilizotengenezwa na Apple Inc. Simu hizi ni mwendelezo wa matoleo ya simu za  iPhone. iPhone 6 na 6 plus zimeingia mtaani taangu Septemba 19, 2014.

iPhone 6 ni mfululizo na mrithi wa iPhone 5s.  Simu hii imeboreshwa zaidi na inamabadiliko mengi ukilinganisha na iPhone 5s. Simu hii imebuniwa kwa kuwa na muonekano mzuri; ina skrini kubwa zaidi zenye inchi 4.7 na 5.5; kifaa cha uchakataji (processor) kina kasi zaidi na imeboreshwa kwenye mfumo wake wa wifi.

Simu hii ilipotoka iliwindwa sana na wapenzi wengi duniani kote na kwa masaa 24 baada ya kutoka watu milioni 4 waliweka oda ya simu hiyo. Huko London na miji mingine wateja walikesha usiku kucha wakipanga foleni kusubiri ufunguzi wa maduka ya apple siku yaa pili yake ili kujipatia simu hii. Wapo waliopanga foleni ili kuwa wa kwanza kununua simu hii, ili waweke historia.

Je simu hi inaubora gani ukifananisha naa simu nyingine za kisasa, Je ina ubora kama zadi ya Samsung?

Kitu cha kwanza utakachokumbana nacho kwenye simu mpya ya Iphone 6 ni muonekano wake kwenye kiyoo chake. Ukubwa wa kioo chake ni zaidi ya toleo lililopita. Iphone 5s inaukubwa wa Inchi 4 na sasa iPhone 6 ina inchi 4.7 na 5.5.

Kwa mujibu wa Dr. Raymond Soneira wa Display Mate aliyefanya majaribio linganifu kwa kuangalia ni jinsi gani Apple wameboresha muonekano wa kioo kwa kutofutisha na toleo la

iPhone 5 lililotolewa 2012, Iphone 6 na iPhone 6 plus zina LCD mzuri zaidi kwenye soko la simu za kisasa.

Katika utafiti huo wa kulinganisha aina za simu na ubora wake iPhone 6 ilichukua nafasi ya pili kwa kupata alama za kijani kwenye maeneo yote yaliyoangaliwa na hivyo kupewa alama ya “Mzuri Sana” kuelekea kwenye alama “Bora”.

Maeneo yaliyoangaliwa kugundua uzuri wake ni pamoja na muonekano wa kioo chake, jinsi ambavyo skrini inaonekana kwa mbali na mchanganyiko wa rangi ya kinachoonekana kwenye kioo.

Pamoja na kwamba Soneira aliisifia skrini ya iPhone 6 wakati wa majaribio, amesema kuwa bado haijaweza kuchukua nafasi ya mshindi wa jumla wa skrini kwa simu za kisasa ambayo ni Samsung Galaxy Note 4.

Samsung Note 4 inatumia skrini yake kwa muonekano tofautitofauti ukilinganisha na simu mpya ya iPhone 6. Pia skrini ya Samsung inatumia OLED na apple inatumia LCD. Samsung Note ni kubwa zaidi ina inchi 5.7 na muonekano wa uzuri wa picha nizaidi ya iPhone 6.

Soneira matokeo ya uchunguzi wake pia umezibitisha kuwa Galaxy Note 4 imevunja rekodi kwa simu za kisasa, katika vipengele vya kuwa na picha halisi ya hali ya juu, muonekano mzuri kwenye skrini na kuwa na mwanga mzuri.

Pamoja na kwamba apple wamekuja kivyao kwenye soko la simu za kisasa kwa ‘muonekano bora’ wa aina yake, Soneira anamini muonekano wa skrini ya Galaxy Note 4 ni bora kama mshindi wa jumla.

Makala hii imeandaliwa na Benedict Kimbache

error: Content is protected !!