May 21, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mume wa Malikia Elizabeth afariki dunia

Prince Pillip

Spread the love

 

MWANAMFALME Phillip (99), mume wa Malkia Elizabeth wa Uingereza, amefariki dunia asubuhi ya leo Ijumaa tarehe 9 Aprili 2021. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Kifo hicho kimetangazwa na Malkia Elizabeth ambapo taarifa yake imechapishwa katika ukurasa wa twitter wa Ikulu ya Buckingham, nchini humo.

Taarifa hiyo imeeleza “kwa masikitiko makubwa Mheshimiwa Malkia Elizabeth anatangaza kifo cha mume wake mpendwa, Mheshimiwa Mwanamfalme Phillip, mtawala wa Edinburg.”

Mtawala huyo wa Edinburgh, amefariki dunia asubuhi ya leo katika makazi ya kifalme yaliyopo Windsor Castor.

Mwanamfalme huyo alizaliwa katika Kisiwa cha Corfu tarehe 10 Juni 1921, ambapo baba yake alikuwa Mwanamfalme Andrew wa Ugiriki na Denmark. Mama wa mwanamfalme huyo alikuwa Mwanamfalme Alice.

Hayati Philip na Elizabeth walifunga ndoa mwaka 1947, ambapo miaka mitano baadaye Elizabeth alitawadhwa kuwa Malkia wa Uingereza.

Wawili hao wamejaaliwa kuwa na watoto wanne, wajukuu wanane na vitukuu 10. Kijana wao wa kwanza alikuwa Charles aliyezaliwa 1948, akifuatiwa na dada yake, Anne (1950), kisha Andrew (1960) na mwisho Edward (1964).

error: Content is protected !!