July 31, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mulongo ampuuza Kigwangala

Spread the love

MAGESA Mulongo, Mkuu wa Mkoa wa Mara, amepuuza tuhuma zilizotolewa na Khamis Kigwangala, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, kwamba, ameaibisha fani ya uuguzi nchini, anaandika Moses Mseti

Bila kumtaja jina Kigwangalwa, Mulugo amesema anashangaa kuona baadhi ya viongozi wakubwa nchini wakimtuhumu na kumtupia lawama baada ya kuwachukulia hatua wauguzi waliosababisha vifo vya mama na mapacha Jijini Mwanza.

Mulongo ametoa kauli hiyo jana wakati akikabidhi ofisi kwa John Mongella, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, aliyehamishwa kutoka Kagera.

Siku chache zilizopita Kigwangala alimtuhumu Mulongo kwamba anaaibisha fani hiyo.

Mulongo akiwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Machi 3 na 6 mwaka huu alisimamisha zaidi ya wauguzi 10 wa Hospitali ya Mkoa huo – Sekou Toure – na Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana kwa madai ya uzembe uliosababisha vifo vya mama na mapacha.

Mulongo amesema, kiongozi haangalii fani ya mtu bali anatekeleza wajibu na kiapo cha uongozi.

Amesema kuwa kiongozi yeyote makini na anayefahamu wajibu wake, hataweza kuangalia fani na badala yake atachakua hatua kwa uzembe uliofanywa na wauguzi hao ili hatua zaidi zikifuatwa.

“Kama kiongozi nisingeweza kuangalia kwamba naingilia fani wala kuihabisha, nilichofuata ni kuona ukubwa wa tukio lenyewe na kufuata kiapo cha uongozi, nashangaa kuona maneno maneno kwamba naingilia fani.

“Na ninawaambiwa kwamba mimi siwezi kuangalia fani za watu na tukianza kuangalia fani za watu hatuwezi kutafanya kazi, wale wanaosubili kuangalia fani za watu wasubiri tu,” amesema Mulongo.

Mongella alimhakikishia Mulongo kuwa, taarifa zilizowasilishwa na tume ilioundwa kuchunguzi matukio mawili ya vifo vya mapacha na mama kwenye hospitali mbili ya mkoa huo na ile ya Wilaya ya Nyamagana anazifanya kazi.

error: Content is protected !!