July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mulongo: Mauaji ya Albino iwe mwisho

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo

Spread the love

MKUU wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo, amewataka watu wanaowaua na kuwakata viungo wenye ulemavu wa ngozi (Albino) kuacha mara moja. Anaandiaka Moses Mseti …. (endelea).

Mulongo alitoa kauli hiyo juzi wakati wa maazimisho ya kwanza Duniani kwa watu wenye ulemavu wa ngozi, kitaifa yaliofanyika Arusha na Kanda ya Ziwa yalifanyika Sengerema mkoani Mwanza.

Amesema, mauaji ya Albino yamekuwa yakifanywa na vikundi vya watu wachache ambao wanaamini imani za kishirikina kwamba, kuuwa albino hutajirika na kuwatahadharisha kuacha vitendo hivyo.

Mulongo ambaye aliwakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Zainab Taraki amesema kuwa, bado wanaendea na uchunguzi wa kuwabaini watu wanaofanya vitendo hivyo na kwamba wakibainika watachukuliwa hatua za kisheria.

Pia amesema, viongozi wa dini wanapaswa kukemea mauaji hayo na kuwahasa waumini wao kuwa mabalozi wa kupinga mauaji hayo.

“Tunapaswa kuwathamini ndugu zetu kwani na wao ni watu kama sisi na tukiachana na mambo hayo, tutawapa nafasi ya wao kufanya kazi kwa amani.

“Mauaji haya yanatuaibisha mkoa wetu na kuhaibisha taifa letu, tunapaswa kuacha mambo haya na kufanya mambo ambayo ni ya msingi,” amesema Taraki.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishina Mwandamizi Msaidizi, Charles Mkumbo, amesema Kanda ya Ziwa inaongoza kwa mauaji hayo na kwamba, jamii inapaswa kulani kitendo hicho.

Amesema, waganga wa kienyeji wanaopiga ramli chonganishi wamekuwa chanzo cha mauaji na kupiga marufuku upigaji ramli na kwamba wananchi wanapaswa kutoa taarifa pindi wanapowatilia shaka watu hao.

Mwaasisi na Mkurugenzi wa Shirika la Under the Same Sun, Peter Ash amesema, walemavu wamekuwa wakitengwa na kusababisha waishi kwa hofu na kushindwa kufanya shughuli zao kwa amani.

Amesema, kuwatenga Albino hakuathiri wao pekee bali ni jamii nzima inaathirika hivyo kila mtu anao wajibu wa kulani mauaji ya aina hiyo yasiendelee kutokea hapa nchini.

“Tutaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania kadri ya uwezo wetu, tutapambana na vitendo hivyo mpaka yatajapokwisha,” amesema Ash.

error: Content is protected !!