October 23, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mulongo anasurika kipigo, kisa Lowassa

Spread the love

VURUGU zimetekeo katika kikao kilichoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo, kilicho wakutanisha watumishi wa Halmshauri ya Kwimba pamoja na walimu wa shule za msingi wilayani humo. Anaandika Moses Mseti, Kwimba … (endelea).

Vurugu hizo zilitokea wakati Mulongo akizungumza watumishi hao wa umma, ghafla kulizuka minong`ono iliyotokana na mkuu huyo kumnanga, Mgombea Urais wa Chadema anayeungwa na mkono na Ukawa, Edward Lowassa.

Inadaiwa kuwa baada ya watumishi hao kubaini mkuu huyo wa mkoa hakuwa na ajenda yeyote inayohusu changamoto zinazowakabili bali ni kampeni za CCM ndipo ilianza minong`ono iliyosababisha kikao hicho kuvunjika.

Akizungumza na gazeti hili kwa sharti la kutotajwa jina lake, mwalimu mmoja amesema kuwa kilichosabisha wao kuanza vurugu ni kutokana na Mulongo kuanza kampigia kampeni mgombea Urais wa CCM, John Mgafuli.

Amesema wakati akiendelea kumfanyia kampeni mgombea huyo, huku akimnanga Lowassa kwa lugha za kejeli ndipo walimu hao walitaka kuuliza maswali ni kwanini anatoa lugha hizo, ambako Mulongo aling`aka na kusema kwamba ni maelekezo na kwamba hakuna maswali.

“Watu walipogundua kwamba hakuwa na ajenda yeyote zaidi ya kutukana Lowassa, ndipo vurugu zilianza na tulipotaka mkuuliza maswali alikataa, kila mtu anaitikadi zake na watu wamelipa nauli zao kufika kwenye kikao,” amesema Mwalimu huyo.

Mtoa taarifa huyo amesema kuwa wakati vurugu hizo zikiendelea, Mulongo aliagiza Polisi ambao walifika na kumkamata mtumishi mmoja ambaye inadaiwa alilala rumande.

Mkuu huyo wa Mkoa, Magesa Mulongo alipotafutwa na gazeti hili kuzungumzia vurugu hizo, amesema kwamba yeye hafanyi kazi katika Halmshauri hiyo na kwamba huo ni upuuzi mtupu.

Mkuu wa Wilaya ya Kwimba, Pili Moshi, yeye alipozungumza alidai kwamba yupo nje ya ofisi na kwamba hawezi kuzungumzia suala hilo na kumtaka mwandishi kumtafuta Jumatatu ya wiki ijayo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kwimba (OCD, Athuman Mkilindi alipotafutwa kuzungumzia tukio hilo, alidai kuwa yeye sio msemaji wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza huku akiishia kusema: “Ndugu suala si linafahamika, muulize RPC (Kamnada wa Polisi Mkoa), Charles Mkumbo.”

error: Content is protected !!