May 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mukoko, Feisal, Sarpong kurejea Uwanjani dhidi ya Simba

Mukoko Tonombe mchezaji wa klabu ya Yanga

Spread the love

WACHEZAJI watatu wa klabu ya Yanga, Feisal Salum, Tonombe Mukoko pamoja na Michael Sarpong watarejea Uwanjani kwenye mchezo ujao wa Ligi Kuu dhidi ya Simba mara baada ya kumaliza kutumikia adhabu ya kadi tatu za njano. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchezo huo wa (Derby) utachezwa Tarehe 8 Mei 2021 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam majira ya saa 11 jioni.

Feisal Salum mchezaji wa klabu ya Yanga

Wachezaji hao watatu wanarejea Uwanjani mara baada ya kukosekana kwenye mchezo uliopita wa hatua ya 16 bora kwenye kombe la Shirikisho (FA) dhidi ya Tanzania Prisons ambao Yanga waliibuka na ushindi wa bao 1-0.

Kwa mujibu wa kanuni za mashindano za Shirikisho la Mpira wa Miguu TFF n ahata shirikisho la Mpira wa Miguu ulimwenguni FIFA kuwa endapo mchezaji atapa kadi tatu kwenye michezo mitatu mfululizo basi atalazimika kukosa mchezo unaofuata.

Watatu hao wanarejea Uwanjani huku wakiwa wachezaji muhimu kwenye kikosi cha Yanga ambao watampa unafuu kocha Nasreddine Nabi kuelekea kwenye mchezo huo.

Michael Sarpong, mshambuliaji wa klabu ya Yanga

Yanga wanakwenda kwenye mchezo huo wakiwa kwenye nafasi ya pili wakiwa na pointi 57 mara baada ya kucheza michezo 27, huku wapinzani wao Simba wakiwa kileleni kwa pointi 61, kwa kucheza michezo 27 mechi mbili nyuma ya Yanga.

error: Content is protected !!