May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mukoko atimkia Mazembe, Yanga yampa mkono wa kwaheri

Spread the love

 

KIUNGO mkabaji Raia wa Jamhuri ya Congo, Mukoko Tonombe amekamilisha usajili wake na kijiunga na klabu ya Tp Mazembe ya nchini mwao, mara baada ya kuhudumu ndani ya klabu ya Yanga kwa mwaka mmoja na nusu. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mukoko ambaye alijiunga na Yanga kwenye msimu wa 2019/20, ameondoka ndani ya klabu ya Yanga huku akiwa amebakiza mkataba wa miezi sita, kufuatia kukosa nafasi ndani ya kikosi cha kwanza.

Taarifa ya kuondoka kwa mchezaji huyo imetolewa na klabu ya Yanga hii leo tarehe 24 Januari 2022, ikimtakia kila la kheri aliyekuwa nahoza wao msaidizi katika klabu yake mpya ya Tp Mazembe.

Mchezaji huyo anaondoka ndani ya klabu ya Yanga, huku akiwa na tuzo ya kuwa mchezaji bora wa klabu hiyo kwa msimu uliopita, kutokana na kucheza idadi nyingi ya mechi na kuonesha uwezo mkubwa.

Tangu kuanza kwa msimu mpya wa 2020/21, Mukoko amepata nafasi ya kuanza kwenye mchezo mmoja wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Pengine usajili wa Khalid Aucho na Yanick Bangala, umemfanya Mukoko kuwa na wakati mgumu ndani ya klabu hiyo, kutokana na ubora waliouonesha wachezaji hao toka walipojiunga na timu hiyo.

error: Content is protected !!