Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Muigizaji Jussie Smollett ahukumiwa jela siku 150
KimataifaMichezo

Muigizaji Jussie Smollett ahukumiwa jela siku 150

Jussie Smollett akipelekwa gerezani
Spread the love

 

MAHAKAMA nchini Marekani imemuhukumu mwigizaji, Jussie Smollett, kifungo cha siku 150 jela ,baada ya jopo la majaji kugundua kuwa alidanganya polisi kuhusu kuwa mtuhumiwa wa uhalifu wa chuki. Anaripoti mwandishi Wetu … (endelea).

Mwanaume huyo ambaye ni nyota wa zamani wa Empire ,mwenye umri wa miaka 39 alipatikana na hatia mwezi Desemba 2021 kwa mashitaka matano ya kufanya fujo, baada ya kutoa taarifa za uongo kuhusu shambulio hilo.

Adhabu hiyo iliyotolewa inajumuisha miezi 30 ya muda wa uangalizi na kulipa dola 145,000 kama marejesho na faini.

Kwa mujibu wa Smollett alikanusha mashitaka hayo nakusema ‘’sikufanya hivyo’’ kesi hiyo ilitokana na tukio la miaka mitatu iliyopita ambapo alisema alishambuliwa na watu wawili.

Jussie Smollett

Muigizaji huyo ambaye ni mweusi na mpenzi wa jinsia moja alisema washambuliaji walimzomea na kauli mbiu ya Tramp, wakamtupia ‘dutu ya kemikali’ na kumfunga kitanzi shingoni alipokuwa akitembea usiku wa manane Januari 2019.

Mamlaka ilifanya uchunguzi, lakini mnamo Februari mwaka huu, polisi walimshitaki Smollett kwa kuwasilisha ripoti ya uongo kwa polisi, akidai hajafanya shambulio hilo.

Katika kesi ya mwaka jana, jopo la wanasheria wanaume sita na wanawake sita, ilisikiliza ushaidi kutoka kwa Abimbola, Olabinjo na Osudairo, ambao walitoa ushahidi kwamba Smollett aliwalipa kuandaa shambulio hilo kwa dola 3,500.

Smollett alikabiliwa na kifungo cha miaka mitatu jela, kwa kila moja ya makosa matano. Siku 150 za kwanza za kipindi chake cha uangalizi kitawekwa kizuizini, kuanza mara moja.

Hata hivyo, lazima alipe dola 120,106 kwa jiji la Chicago na dola 25,000 kama faini kiwango cha juu kinachoruhusiwa na sheria.

Wakati wote wa kesi hiyo, Smollett alishikilia kuwa alikuwa mwathirika wa uhalifu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaKimataifa

Mwanaye rais jela miaka miaka 6 kwa dawa za kulevya

Spread the loveMwanawe rais wa zamani wa Guinea-Bissau amehukumiwa kifungo cha miaka...

Habari za SiasaKimataifa

Faye aahidi kuongoza kwa unyenyekevu, wagombea wenzie wakubali yaishe

Spread the loveMgombea wa upinzani Senegal, Bassirou Diomaye Faye anajiandaa kuwa rais...

Habari MchanganyikoKimataifa

Wanafunzi 130 waliokuwa wametekwa nyara waokolewa

Spread the loveZaidi ya wanafunzi 130 wa shule ya msingi LEA na...

error: Content is protected !!