June 17, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Muhimbili yapeleka wataalamu India

Jengo la Hospitali ya Taifa ya Muhimbili

Spread the love

WATAALAMU 20 wa fani mbalimbali wa Hopitali ya Taifa Muhimbili (MNH), wameondoka nchini kwenda nchini India kupata elimu kwa ajili ya kujengewa uwezo wa upandikizaji figo kwa watu wenye matatizo ya figo, anaandika Penndo Omary.

Wataalamu hao wameondoka wiki iliyopita ambapo pamoja na mambo mengine watapata mafunzo ya kuwawezesha kufanya upasuaji na upandikizaji wa figo.

Taarifa iliyotolewa leo na Dk. Hedwiga Swai, Mkurugenzi wa Tiba wa MNH, imesema wataalamu hao ni; madaktari bigwa wa upasuaji na upandikizaji figo, madaktari bingwa wa magojwa ya figo, wataalamu wa maabara, madaktari wa usingizi na madaktari wa chumba cha wagojwa wanaohitaji uangalizi maalum.

Wengine ni wataalam wa mionzi, wauguzi wa chumba cha upasuaji na chumba cha wagojwa wanaohitaji uangalizi na wataalam wengine ambao wanakwenda kujifunza.

“Suala la mgojwa kupandikizwa figo ni mchakato na haliwezekani kufanywa na mtu mmoja. Ni kazi inayowahusisha wataalamu wengi. Watakaa mafunzoni kwa muda wa miezi mitatu na shughuli za upasuaji na upandikizaji figo zitaanza Januari mwakani,” amesema Dr. Swai.

Aidha, Dk. Swai amesema upandikizaji figo utapunguza rufaa za wagojwa kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kupatiwa matibabu na kuokoa fedha nyingi za serikali za kuwapeleka wagojwa nje ya nchi.

error: Content is protected !!