Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Mufti Zubeir: Tunachonganishwa
Habari Mchanganyiko

Mufti Zubeir: Tunachonganishwa

Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir
Spread the love

SHEIKH Abubakar Zubeir, Mufti Mkuu wa Tanzania ‘amelalamikia’ kuchongwanishwa kwa Baraza Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata) na serikali. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Amesema, (bila kutaja jina ama taasisi) watu hao wanaidai taasisi hiyo (Bakwata) inaipotosha serikali bila kufafanua madai hao.

Malalamiko hayo ameyatoa wakati akihutubia kwenye Swala ya Eid El Adha iliyofanyika kitaifa katika viwanja vya Msikiti wa Kibadeni, Chanika Jijini Dar es Salaam.

waonya baadhi ya watu wanaolichonganisha Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) na serikali.

Ingawa hakueleza kwa undani ‘uchonganishi huo’ lakini mwishoni mwa wiki, kumekuwa na malalamiko kwamba taasisi hiyo haisemi kweli kuhusu siku mahususi ya Eid El Adha ambapo hutanguliwa na funga ya Arafa.

Kwa kawaida, Waislam kote duniani hufunga siku ya Arafa (Siku ambayo mahujaji husimama Arafa), ambayo ilikuwa Jumamosi na hivyo, siku inayofuata (Jumapili) huwa Eid.

Hivyo, madai ya Bakwata kuipotosha serikali yameibuka baada ya taasisi hiyo kutangaza Eid El Adha siku ya Jumatatu badala ya Siku ya Jumapili.

Akizungumza kwenye swala hiyo ya Eid Mufti Zubeir amewataka watu wasio wasemaji wa Waislam kuacha kuwasemea na kwamba, hatovumilia Bakwata kuvunjiwa heshima.

Amesema, inapaswa kila mtu awe na mipaka sambamba na kuheshimu mamlaka za wengine.

“Bakwata haivumilii tena kunyanyaswa, kuvunjiwa heshima, adabu na mtu yeyote. Niwaelekeze Waislamu kwamba, kila watu wana msemaji wao, wewe unaweza kuwa msemaji wa taasisi yako lakini huwezi kuwa msemaji wa Waislamu wote Tanzania,” amesema Mufti Zubeir na kuongeza:

“Huwezi mtu anasema kwamba serikali inapotoshwa, mnataka kuichonganisha baraza na serikali? Ili serikali ione inapotoshwa na hawa, tunaiambia serikali kwamba, hatuipotoshi.”

Suleiman Jaffo, Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI akizungumza katika tukio hilo, amewataka Watanzania kuienzi na kuilinda amani kwasababu nchi isiyo na amani, haina maendeleo.

“Watanzania tujielekeze sana katika suala la amani kwasababu kuna wengine wana nia ovu, wanaweza kutumia utaratibu wa aina yoyote kupoteza Amani, ukipoteza amani umevunja uchumi wa nchi husika,” amesema Jaffo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Puma Energy Tz: Watanzania tudumishe amani kuvutia uwekezaji

Spread the loveKAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imewakutanisha wadau mbalimbali katika...

Habari Mchanganyiko

DAWASA waanza utekelezaji agizo la Samia

Spread the loveMamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

error: Content is protected !!