June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mufti Zubeir alazwa

Spread the love

ABUBAKAR Zuberi, Mufti wa Tanzania kupitia Baraza Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata), amelazwa kwenye Hospital ya Taifa ya Muhimbili kwa ugonjwa wambao haujatajwa. Anaandika Faki Sosi.

Taarifa kutoka ndani ya Bakwata zinaeleza kuwa, Mufti Zuberi alifikishwa Muhimbili jana baada ya kuugua ghafla.

Saidi Mpeta ambaye ni Ofisa Habari wa Bakwata amethibitisha kulazwa kwa Mufti Zuberi na kwamba alifikishwa Muhimbili jana.

Hata alipoulizwa ugonjwa unaomsumbua Mufti Zuberi, Mpeta hakutaka kuweka wazi ugonjwa huo na kudai taarifa itatolewa. Mufti Zuberi alichakuliwa kuwa Mufti wa Tanzania tarehe 10 Septemba mwaka jana.

error: Content is protected !!