Sunday , 5 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Mufti aunda Tume ya watu saba kuchunguza mali, madeni ya BAKWATA
Habari Mchanganyiko

Mufti aunda Tume ya watu saba kuchunguza mali, madeni ya BAKWATA

Spread the love

 

MUFTI na Sheikh Mkuu wa Tzania, Sheikh Dk. Abubakar Zubeir, ameunda tume ya watu saba kwaajili ya maboresho ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), ambapo pamoja na mambo mengine itafanya uchunguzi wa mali za baraza hilo zinazomilikiwa na watu wengine kinyume na taratibu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salam … (endelea).

Mufti Zubeir amesema amechukua hatua hiyo kwa mujibu wa Katiba ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kipengele 84:17 na kuipa hadidu za rejea sita za kufanyia kazi ikiwemo pia kuhakiki madeni ya Bakwata na kushauri namna ya kuyalipa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mufti leo Ijumaa tarehe 20 Januari, 2023, Tume hiyo inaundwa na Sheikh Issa O. Issa ambaye ni Mwenyekiti, Alhaji Omar Ege ambaye ni Katibu na wajumbe ni Alhaji Mruma, Daudi Nasibu, Iddi Kamazima, Mohamed Nyengi na Qassim Jeizan.

Hadidu zingine za rejea ni pamoja kufanya tathimini ya changamotop za mifumo ya utawala inayoikabili Bakwata na kushauri namna bora ya kufanya maboresho.

Pia Tume itafanyauchunguzi wa mikoa na wilaya zenye migogoro mikubwa ya uopngozi au mali na kuchukua hatua kuitatua, kuibua na kubuni vyanzo vipya vya mapato kwa Bakwata na masuala mengine muhimu ambayo Tume itaona yanafaa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Haya hapa majina 12 ya familia moja waliofariki kwenye ajali Tanga

Spread the love  MAJINA 12 kati ya 17 ya waliofariki dunia katika...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia awalilia 17 waliofariki ajalini wakisafirisha maiti

Spread the love  RAIS Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kwa...

Habari Mchanganyiko

Wanawake wachimbaji wajenga zahanati kuokoa afya za wakazi 2000

Spread the love  ZAIDI wakazi 2,000 wa kijiji cha Nyamishiga Kata ya...

Habari Mchanganyiko

Baada ya Congo DR, Somalia mbioni kujiunga na EAC

Spread the love  TAIFA la Somalia liko mbioni kuwa mwanachama rasmi wa...

error: Content is protected !!