NAIBU Waziri wa Nishati, Stephen Byabato amesema marekebisho ya kanuni za utengenezaji na uwekaji vituo vya mafuta katika maeneo ya vijijini, yanatarajiwa kukamilika Mei 2022. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha…(endelea).
Byabato ametoa taarifa hiyo akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa wiki ya maji, iliyofanyika jijini Arusha, ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais, Dk. Phillip Mpango.
Amesema marekebisho hayo yatapelekea vituo vya uuzaji mafuta vijengwe kwa wingi maeneo ya vijijini, ambapo imependekezwa gharama zake zisizidi Sh. 7,000,000.
“Tunafanya mpango wa kurekebisha kanuni za utengenezaji na uwekaji vituo vya mafuta katika eneo la vijiji, ili kuhakikisha usalama wao ambao kwa sasa wanauza mafuta katika vidumu vya maji, waweze kupata vituo kwa gharama nafuu kwenye maeneo yao,” amesema Byabato na kuongeza:
“Kufikia Mei tutakuwa tumekamilisha kanuni na tungetamani na kupenda angalau kituo kinachowekwa katika maeneo ya vijijini kisigharimu zaidi ya Sh. 7 milioni ili huduma iwafikie wengi.”
Leave a comment