August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mtuhumiwa wa kuiba mil 7 kwa dakika apandishwa kizimbani

Spread the love

MOHAMEDI Mustafa Mkurugenzi wa Kampuni ya Farm Plant Limited na wenzake wanne wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kuisababishia serikali hasara ya Sh 15.6 billion, anaandika Faki Sosi.

Watuhumiwa wengine ni  pamoja na Alloycious Mandogo, Isaack Kasanga, Taherali Taherali, na Mohammed Kabura.

Akiwasomea mashitaka Shadrack Kimaro wakili wa serikali mkuu, katika kesi hiyo namba 28 ya mwaka 2016 mbele ya Huruma Shahidi Hakimu katika Mahakama hiyo amedai kuwa katika kesi hiyo mtuhumiwa namba moja Mustafa anatuhumiwa kwa makosa 199.

Katika mashitaka hayo mtuhumiwa shitaka namba 197 mtuhumiwa  namba moja (Mustafa) anatuhumiwa kukwepa kodi yenye thamani ya Sh. 15.6 Billioni akiwa kama mkurugenzi wa kamapuni hiyo.

Katika shitaka namba 198 linawakabili watuhumiwa wote ambapo wanatuhumiwa kutakatisha fedha zaidi ya Sh. 1 bilioni walizopitaka kwa njia haramu na kuzitakatisha.

Shitaka la Mwisho linamkabili  mtuhumiwa namba moja (Mustafa) la kuisababishishia serikali hasara  zaidi ya Sh. 15.6 bilioni.

Mashtaka mengine ambayo anashitakiwa nayo (Mustafa) kwa kughushi nyaraka za uongo na kuziwasilisha katika Ofisi za Mamlaka ya Mapato katika mkoa wa Kodi wa Kinondoni Jijini Dar es Salaam kwa nyakati toufauti kuanzia mwaka 2013 na kusajili kampuni kadhaa kama kampuni zisizo kuwa zina uhalali nchini na kufanya ulaghai kwa mamlaka ya mapato.

Hakimu Shihidi amesema kuwa kutokana na tuhuma za kuhujumu uchumi watu hao hawataweza kuiyambia chochote mahakama hivyo wamekosa dhamana na kurudishwa lumande kesi hiyo itatajwa tena tarehe 25 Julai mwaka huu.

 

error: Content is protected !!