November 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mtuhumiwa ulawili wa mtoto na kumsababishia kifo mbaroni

Kamanda Polisi wa Kanda ya Dar es Salaam, Jumanne Murilo

Spread the love

 

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam nchini Tanzania, linamshikilia mtu mmoja mwenye umri wa miaka 16 kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wa miaka minne na baadaye kupoteza maisha. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi tarehe 11 Novemba 2021 na Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Jumanne Muliro amesema, mtuhumiwa huyo jina linahifadhiwa kwa sasa.

Kamanda Muliro amesema, tukio hilo lilitokea jana Jumatano, tarehe 10 Novemba 2021 saa 3 asubuhi maeneo ya Chamazi Mbande wilaya ya Temeke.

“Uchunguzi wa kina juu ya tukio hilo unafanyika na hatua za kisheria wakati wa uchunguzi zitazingatiwa ili haki itendeke,” amesema Muliro

error: Content is protected !!