
Mtuhumiwa katika kesi ya uhujumu uchumi, Harbinder Sethi
HATIMAYE mtuhumiwa katika kesi ya uhujumu uchumi, Harbinder Sethi amepata ruhusa ya kwenda kutibiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH). Anaandika Faki Sosi.
Ruhusa ya mtuhumiwa huyo kupelekwa Muhimbili umetolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Awali Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ilizuia mtuhumiwa huyo kwenda kutibiwa Muhimbili.
Hakimu Huruma Shahidi alipokea maelezo ya Mwendesha Mashtaka Mwandamizi wa Takukuru, Leonard Swai kwamba tayari Takukuru amepelekwa Muhimbili na kwamba kinachosubiriwa ni ripoti ya daktari.
More Stories
Mapadri 25, Masista 60 waaga dunia Tanzania
TCRA yajitosa bei za vifurushi
Huawei yaunga mkono malengo endelevu UN