July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mtoto wa Rais mstaafu afungwa kwa rushwa

Mtoto wa Rais wa zamani wa Senegal, Karim Wade

Spread the love

KARIM Wade-mtoto wa Rais mstaafu wa Senegal amehukumiwa kifungo cha miaka sita jela baada ya Mahakama ya nchini humo kumtia hatiani kwa kosa la rushwa.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), Karim Wade pia ametozwa faini ya dola 228 milioni kwa ajili ya utajiri haramu aliojipatia wakati wa utawala wa miaka 12 ya baba yake.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Karim amechaguliwa kuwa mgombea urais wa chama kikuu cha upinzani (PDS).

Rais Macky Sall wa nchi hiyo ameonya wiki iliyopita kwamba serikali yake isingeweza kuvumilia jaribio lolote la kudhoofisha Senegal baada ya mahakama kutoa uamuzi wake.

Rais Sall alimwangusha Abdoulaye Wade katika uchaguzi mkali wa 2012 uliokuwa na ushindani mkubwa.

Karim Wade alishtakiwa kwa kosa la kujipatia dola 1.4 bilioni kinyume cha sheria wakati baba yake alipokuwa madarakani.

Jaji Henri Gregoire Diop alisema kuwa Karim alikuwa ameficha fedha mbali katika makampuni kwenye visiwa vya British Virgin na Panama.

Wafuasi wa upinzani ndani ya chumba cha mahakama walipiga kelele na baadaye kufanya maandamano, kukemea uamuzi huo waliouita wa “aibu”.

Karim Wade alikuwa waziri mwandamizi katika serikali ya baba yake, na alikuwa msimamizi wa miundombinu na miradi ya nishati kubwa.

Karim anadaiwa kupewa makampuni kadhaa ya kigeni kwa njia haramu katika Senegal. Amekuwa kizuizini tangu Aprili 2013.

Kukamatwa kwake kulifanyika baada ya serikali mpya kuapa kupambana na ufisadi.Senegal,

error: Content is protected !!