Tuesday , 5 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mtoto wa Rais Jumbe ajitosa Urais Zanzibar, wagombea wafika 30
Habari za Siasa

Mtoto wa Rais Jumbe ajitosa Urais Zanzibar, wagombea wafika 30

Spread the love

MUSSA Aboud Jumbe, amekuwa mwanachama wa 30 wa Chama cha Mapinduzi (CCM), kuchuchukua fomu ya kugombea Urais wa Zanzibar kupitia chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar…(endelea).

Jumbe ambaye ni Mtoto wa Rais wa awamu ya pili wa Zanzibar, Aboud Jumbe amekabidhiwa fomu hiyo leo Ijumaa tarehe 26 Juni 2020, katika Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui,  na Cassian Gallo’s, Katibu wa Kamati Maalumu ya NEC Idara ya Oganaizesheni Zanzibar .

Akizungumza baada ya kukabidhiwa fomu hiyo, Jumbe amewataka Wazanzibar kumuombea ili afanikiwe katika mchakato huo.

“Nafahamu kabla yangu, wako wengi walishafika kwa ajili ya kupata ridhaa ya chama na baada ya hapo kupata ridhaa ya wananchi wa Zanzibar, nisingependa leo kuzungumza mengi sana, niwaombeni tu nanyi muwe pamoja nami,” amesema Jumbe

“Mniunge mkono katika kuniombea kwa Mungu lililokuwa lenye kheri liweze kufikia pale inapostahiki, baada ya hayo nisingelipenda kuzungumza zaidi,” amesema

Jumbe amekuwa mtoto wa tatu wa marais wastaafu kujitokeza kuchukua fomu ya kugombea urais wa Zanzibar,  baada ya Dk. Hussein Mwinyi, Mtoto wa Rais Mstaafu wa Tanzania, Dk. Ali Hassan Mwinyi na Balozi Ali Abeid Karume, Mtoto wa Rais Mstaafu wa Zanzibar, Hayati Abeid Amana Karume.

Tangu zoezi la uchukuaji na urudishaji fomu, sambamba na utafutaji wadhamini lifunguliwe tarehe 15 Juni 2020, takribani watu 30 wamejitosa katika mchakato huo, ambapo wanawake waliojitokeza hadi sasa ni watatu na wanaume 27.

Wanawake waliojitokeza ni, Mwatum Mussa Sultan, Hasna Atai Masoud na Fatma Kombo Masoud.

Zoezi hilo linatarajiwa kufika tamati tarehe 30 Juni 2020, majira ya saa 10:00 jioni.

Wagombea wote 30 waliojitokeza ni;

 1. Mbwana Bakari Juma
 2. Balozi  Ali Abeid Karume
 3. Mbwana Yahya Mwinyi :
 4. Omar Sheha Mussa
 5. Dk. Hussein Ali Mwinyi
 6. Shamsi Vuai Nahodha
 7. Mohammed Jaffar Jumanne
 8. Mohammed Hijja Mohammed
 9. Issa Suleiman Nassor
 10. Profesa Makame Mnyaa Mabarawa
 11. Mwatum Mussa Sultan
 12. Haji Rashid Pandu
 13. Abdulhalim Mohammed Ali
 14. Jecha Salum Jecha
 15. Dk. Khalid Salum Mohammed
 16. Rashid Ali Juma
 17. Khamis Mussa Omar
 18. Mmanga Mjengo Mjawiri
 19. Hamad Yussuf Masauni
 20. Mohammed Aboud Mohammed
 21. Bakari  Rashid Bakari
 22. Hussein Ibrahim Makungu
 23. Ayoub Mohammed Mahmoud
 24. Hashim Salum Hashim
 25. Hasna Atai Masound
 26. Fatma Kombo Masound
 27. Iddi Hamadi Iddi
 28. Pereira Ame Silima
 29. Shaame Simai Mcha
 30. Mussa Aboud Jumbe

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Biteko: Viongozi tuache alama nzuri katika utendaji wetu

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Chanzo maporomoko yaliyoua 65 Hanang, chatajwa

Spread the loveSERIKALI imesema kumeguka kwa sehemu ya Mlima Hanang ambao ilikuwa...

Habari za Siasa

Baba yake Ole Sabaya ashinda Uenyekiti CCM – Arusha

Spread the loveLoy Thomas Sabaya ambaye ni Baba wa aliyekuwa Mkuu wa...

Habari za Siasa

Serikali yaagiza uchunguzi chanzo maporomoko Hanang

Spread the loveSERIKALI imeagiza uchunguzi ufanyike ili kubaini chanzo cha maporomoko ya...

error: Content is protected !!