August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mtoto wa Obama aamua kuuza Mgahawa

Spread the love

Sasha Obama mtoto wa Barack Obama rais wa Marekani ameanza kazi ya uhudumu katika Mgahawa mmoja nchini Marekani, anaandika Wolfram Mwalongo.

Sasha mwenye umri wa miaka 15 ameamua kuhudumia wateja katika Mgahawa huo uliopo eneo la Martha’s Vineyard, Massachusetts.

Kwa mujibu wa Gazeti la Boston Herald limesema siku ya kwanza binti huyto kuanza kazi, alisindikizwa na watu sita hali iliyo wafanya watu kugundua  kuwa walikuwa walinzi wake ‘Secrect Service’.

“Tulikuwa tunashangaa ni kwa nini kulikuwa na watu sita walikuwa wanamsaidia msichana huyu, lakini baadaye tukagundua alikuwa nani,” alisema mmoja wa wafanyakazi wa mgahawa huo.

Aidha Familia ya Rais huyo wa marekani imekuwa ikitumia mara kwa mara mgahawa huo hasa kipindi cha likizo.

Picha zimesambaa mitandaoni zikimuonyesha binti huyo akiwa amevalia sare ya kazi na akiwahudumia wateja hali inayoendelea kuzua gumzo katika mitandao.

Hakuna taarifa rasmi iliyotolewa na Rais Obama juu ya uamuzi huyo wa binti yake.

error: Content is protected !!