
Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema
DUDLEY, mtoto wa Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani Tanzania- Chadema, Freeman Mbowe ameshangazwa na tuhuma zinazomkabili baba yake. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Mbowe anashikiliwa na Jeshi la Polisi Tanzania tangu usiku wa tarehe 21 Julai 2021, alipokamatwa jijini Mwanza kisha kusafirishwa hadi Dar es Salaam kwa mahojiano zaidi.
Jana Alhamisi, tarehe 22 Julai 2021, Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, David Misime alitoa taarifa ya kushikiliwa kwa Mbowe akisema, anatuhumiwa kwa tuhuma za kula njama ya kufanya vitendo vya kigaidi ikiwemo kuua viongozi wa serikali.
So when Pres Samia was tweeting condolences for baba mkubwa, she was giving condolences to a known terrorist?
— Dudley (@dude_ly_) July 22, 2021
Mara baada ya taarifa hizo, Dudley kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter, akiandika akihoji “kwa hiyo wakati Rais Samia, anatoa salamu za pole kwa kifo cha baba mkubwa (Charles Mbowe), alikuwa anajua anatoa salamu hizo kwa gaidi?
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, alituma salamu za rambirambi kwa Mbowe baada ya kifo cha kaka yake, Charles kilichotokea tarehe 8 Julai 2021, kupitia ukurasa wake wa twitter.
Nakupa pole Ndg. @freemanmbowetz (Mwenyekiti wa CHADEMA) na wafiwa wote kwa kuondokewa na ndugu yenu mpendwa Charles Mbowe. Nawaombea moyo wa subira, uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki cha majonzi. Bwana ametoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe, Amina.
— Samia Suluhu (@SuluhuSamia) July 8, 2021
Charles alifikwa na mauti katika Hospitali ya KCMC, Moshi mkoani Kilimanjaro, tarehe 8 Julai 2021. Mbowe alisema chanzo cha kifo cha kaka yake kilitokana na maambukizo ya corona.
More Stories
Msukuma: Mbowe alipa-miss Ikulu
Wabunge upinzani, CCM waungana kumpongeza Rais Samia
Dk. Mollel naye aagizwa kujibu maswali kwa ukamilifu