Friday , 3 February 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Mtoto wa Gadafi aachiwa huru, atimkia Uturuki
Kimataifa

Mtoto wa Gadafi aachiwa huru, atimkia Uturuki

Spread the love

 

MTOTO wa tatu wa kiongozi wa zamani wa Libya, Muammar Gaddafi, Al-Saadi Gaddafi (48) ameachiwa huru kutoka gerezani alikokuwa ameshikiliwa kwa miaka saba huko Tripoli nchini Libya. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Mwendesha mashtaka wa Serikali, Abdul Hamid Dbeibeh amesema wizara ya sheria ya nchi hiyo haina nia ya kuendelea kumshikilia Saadi hasa ikizingatiwa kuwa mahakama iliyokuwa inasikiliza kesi yake ilishathibitisha kuwa hana hatia.

Jana Jumapili tarehe 5 Septemba, 2021, Serikali ya Libya ilitoa taarifa ya kuachiwa kwake kutaweza kulisaidia taifa hilo kufikia katika makubaliano.

Saadi aliyekuwa Kamanda wa Kikosi malumu cha Libya, aliwekwa korokoroni tangu mwaka 2014 kutokana na tuhuma za utakatishaji fedha kipindi akiwa Rais Shirikisho la Kandanda kipindi cha uongozi wa baba yake.

Saadi ambaye pia alikuwa mchezaji maarufu wa soka, enzi zake alicheza kandanda katika timu mbalimbali nchini Italia pamoja na timu yake ya Taifa.

Baada ya baba yake kupinduliwa mwaka 2011, Saadi alikimbilia nchini Niger lakini mwaka 2014 alirejeshwa Libya ambako alikutwa hana hatia ya baadhi ya kesi mauaji iliyokuwa inamkabili isipokuwa kesi nhiyo ya utakatishaji fehda.

Hata hivyo, baada ya kuachiwa huru inaelezwa kuwa Saadi ametokomea nchini Uturuki.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Hospitali za China zilifurika wagonjwa, wazee kipindi cha wa likizo ya Mwaka Mpya wa Lunar

Spread the loveHOSPITALI  nchini China zimejaa wagonjwa na wazee katika kipindi cha...

Kimataifa

Papa Francis ayataka mataifa ya nje kuacha kupora mali DRC

Spread the love  KIONGOZI wa kanisa Katoliki Papa Francis, ameyataka mataifa ya...

Kimataifa

Mashabiki wakabiliwa na mashtaka ya mauaji baada ya wafuasi wa Arsenal na Manchester City kupigana Uganda

Spread the love  MASHABIKI wawili wa soka nchini Uganda wanakabiliwa na mashtaka...

Kimataifa

China inatathmini upya sera za wafanyakazi

Spread the love  WAKATI idadi ya watu wa nchi China inapungua, Beijing...

error: Content is protected !!