September 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mtoto apatikana hai chini ya kifusi

Spread the love

MTOTO mwenye umri wa mwaka mmoja amepatika akiwa hai katika jengo la ghorofa sita lililoanguka Jumanne wiki iliyo pita jijini Nairobi ambapo watu 20 walifariki dunia na zaidi ya 90 hawajulikani walipo, anaandika Wolfram Mwalongo.

Pius Maasai, Kamanda wa Kitengo cha Taifa cha Kudhibiti Majanga amesema, mtoto huyo aliokolewa kwenye kifusi saa 10 alfajiri ya leo na kukimbizwa hospitali.

Amesma, hali yake inaendele vizuri na kwamba, juhudi za uokoaji zinaendelea. Mpaka sasa amesema zaidi ya watu 136 tayari wameokolewa.

error: Content is protected !!