March 7, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mtoto afariki kwenye ajali ya moto

Ulrich Matei Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya

Spread the love

MTOTO mmoja aliyefahamika kwa jina la Chriss Shida (2) amefariki dunia baada ya kuungua na moto akiwa nyumbani kwao katika kijiji cha Kimondo Wilayani Mbeya mjini. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza na wanahabari leo tarehe 28 Agosti, 2018 SACP Ulrich Matei, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya amesema tukio hilo lilitokea jana majira ya saa mbili usiku.

Akielezea kuhusu tukio hilo, amesema chanzo cha moto huo ni mabanzi na majani ya jiko kuanguka wakati wahanga wako jikoni wanakula na kusababisha kushika moto na kuwaunguza.

Aidha, Kamanda Matei amesema mama mzazi wa marehemu aitwaye Maria Lucas alijeruhiwa na moto huo sehemu za mikononi na kifuani.

Kamanda Matei amesema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali teule ya Ifisi Mbalizi na mama wa marehemu anapatiwa matibabu hospitalini hapo.

error: Content is protected !!