August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mtoboa macho ‘Scorpion’ huru

Spread the love

SALUM Njwete maarufu kwa jina la Scorpion , kijana aliyemtumbua macho Said Mrisho na baadaye kupandishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam, ameachwa huru, anaandika Wolfram Mwalongo.

Mahakama hiyo imefuta shitaka la unyang’anyi wa kutumia silaha lililokuwa likimkabili Scorpion leo baada ya upande wa mashtaka kuomba liondolewe. Hata hivyo amekamatwa tena.

Scorpion ambaye ni mkazi wa Buguruni Kwa Mnyamani, kwa mara ya kwanza alipandishwa kizimbani tarehe 23 Septemba mwaka huu kwa kutuhumiwa kumtoboa macho Mrisho katika eneo la kituo cha mafuta Buguruni jijini hapa.

Kwa mjibu wa mwendesha mashitaka wa Serikali Munde Kalombola, alidai kuwa tarehe 6 Septemba mwaka huu katika maeneo ya kituo cha mafuta Buguruni, mshitakiwa huyo alimchoma kisu Mrisho tumboni, begani na machoni.

Uamzi huo wa mahakama umekuja ikiwa ni wiki moja tangu Taasisi ya T-Marc Tanzania kupitia Mkurugenzi wake Diana Monika Kisaka kutoa taarifa ya masikitiko kuhusu tukio hilo.

Scorpion alikuwa Mshindi wa Dume Challenge, shindano lililoandaliwa na taasisi hiyo na badaye kuwa balozi wa kondomu (2012- 2014).

error: Content is protected !!