MGOMBEA Urais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), Jeremiah Mtobesya, ameahidi kuimarisha uhuru wa chama hicho pamoja na kuongeza mapato yake, endapo atachaguliwa kushika wadhifa huo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Mtobesya ametoa ahadi hizo leo Jumatano, tarehe 27 Aprili 2022, katika mdahalo wa wagombea urais wa TLS, uliofanyika jijini Dar es Salaam. Wagombea wengine ni, Profesa Edward Hoseah na Harold Sungusia.
“Suala lingine nitakalofanyia kazi ni independence of the bar (uhuru wa chama). Mawakili wenzetu mara nyingi tumewaona wakiingiliwa wakati wanafanya kazi zao, wakati mwingine anakuwa katika mgogoro na sheria bila sababu. Iwapo nitapata wasaa tutahakikisha tunawasaidia wakiwa kwenye mgogoro,” amesema Mtobesya.
Mtobesya amesema “tutatetea haki zao katika mfumo wa kistaarabu kwa kufuata sheria, sababu sheria zipo. Tutahakikisha haki ya wakili inapatikana bila kugandamiza haki yake.”
Aidha, ameahidi endapo atachaguliwa kuwa Rais wa TLS, atahakikisha chama hicho kinatekeleza majukumu yake katika kusimamia Bunge na Mahakama, kwa kutumia mpango kazi wake.
Mtobesya ameahidi endapo atachaguliwa, atasimamia maslahi ya mawakili wachanga.
“Ni ukweli usiopingika wadogo zetu wanapoingia sokoni wana struggle, si suala zuri kuwaacha waendelee ku-struggle, tumeshuhudia wengine wakikiuka maadili ili kuishi, nikichaguliwa tutafanya fund raising waji-organize kwenye vikundi kufungua kampuni kisha baadae watazirejesha ziwasaidie wengine,”a mesema Mtobesya.
Mtobesya ameahidi kufufua taasisi za TLS, ikiwemo Idara ya Maendeleo ya Biashara.
Leave a comment