MAJI ya Mto Ruvuma, yapo kwenye mpango wa serikali kutumika kuzalisha umeme. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Kauli hiyo imetolewa na Jumaa Aweso, Waziri wa Maji leo Jumatatu tarehe 12 Aprili 2021, bungeni jijini Dodoma, wakati akijibu swali la Abdallah Chikota, Mbunge wa Nanyamba (CCM), aliyetaka kujua mpango wa serikali kuhusu hilo.
Chikota ameuliza, ni lini serikali itaanza kutumia maji ya Mto Ruvuma kwa ajili ya kujenga miradi mikubwa ya maji, ambayo itatatua changamoto za maji kwa Jimbo la Nanyamba na maeneo Jirani?
“Mradi wa maji kutoka Mto Ruvuma ni miongoni mwa miradi mikubwa ya kimkakati, serikali inatarajia kuanza utekelezaji wake katika mwaka wa fedha 2021/22 kulingana na upatikanaji wa fedha.

“Kupitia RUWASA, ukarabati na upanuzi wa mradi wa maji kwenye vijiji vya Malongo na Migombani umekamilika na unatoa huduma kwa wananchi, Vilevile, visima viwili (2) vimechimbwa, mtambo nyumba ya mitambo ya kusukuma maji, ulazaji wa bomba kuu kilomita 3.5.
“Ujenzi wa tanki moja (1) la ujazo wa lita 100,000 na ujenzi wa matanki mengine manne (4) unaendelea,” amesema waziri huo.
Amesema, utekelezaji wa miradi katika vijiji vya Ngonja – Chawi, Mayembejuu, Nyundo A na B, Nitekela na Misufini upo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.
Leave a comment