May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mtifuano VPL

Kikosi cha timu ya Namungo FC

Spread the love

 

LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inaendelea tena leo kwa michezo mitatu kupigwa kwenye viwanja tofauti ambapo Azam FC atakuwa ugenini Shinyanga kucheza dhidi ya Mwadui FC. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezo mwingine utakuwa Kagera Sugar dhidi ya Namungo FC utakaopigwa kwenye Uwanja wa Kaitaba, huku Ruvu Shooting akiwa nyumbani atawaalika JKT Tanzania.

Michezo hiyo ni muhimu kwa kila timu Mwadui FC yupo chini kwenye msimamo anahitaji kupata ushindi ili ajikwamue kushuka daraja wakati huo Azam FC wakipambana kuongeza pointi ili kuwakaribia Yanga na Simba ambao wapo juu yao kwenye msimamo.

Kagera Sugar wakiwa kwenye nafasi ya 13 wanahitaji kufanya vizuri kwenye mchezo wao dhidi ya Namungo FC ambao unaonekana kuwa mgumu ili kujiondoa kucheza mechi za mtoani (Play Off) na timu kutoka daraja la kwanza.

Ligi hiyo mpaka sasa imechezwa jumla ya michezo 22 kwa baadhi ya timu ambapo klabu ya Yanga licha ya kupoteza mchezo wao uliopita dhidi ya Coastal Union wanaendelea kusalia kileleni wakiwa na pointi 49.

Nafasi ya pili inashikiliwa na Simba ambayo imecheza 19, wakiwa na pointi 45 wakiwa na michezo mitatu mkononi.

Timu hizo mbili kwa sasa zinapewa nafasi kubwa kutwaa taji la Ligi kutokana na ushindani uliokuwepo kwa sasa na kufanya vizuri kwa vikosi vyao.

Vita hiyo ya Ligi haishii hapo tu inashuka mpaka kwenye timu sita za chini kwenye msimamo huo ambazo zipo hatalini kushuka daraja.

Nafasi ya mwisho kwa sasa inashikwa na Mwadui FC ambayo inapointi 15 mara baada ya 22, huku juu yao wakiwa Mbeya City yenye pointi 16 baada ya kucheza michezo 21.

Baada ya kufanya vizuri kwenye michezo ya hivi karibuni Ihefu imepanda mpaka nafasi ya 16 wakiwa na pointi 20 baada ya kucheza michezo 22, huku Gwambina wakiwa kwenye nafasi ya 15 wakiwa na pointi 23.

Timu zote hizo nne zipo kwenye hatari ya kushuka daraja huku mbili zikienda kucheza mtoano (Play off) na timu za daraja la kwanza kwa kupigwa michezo nyumbani na ugenini.

error: Content is protected !!