July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mtifuano kufuzu fainali kombe la Dunia

Spread the love

 

Kuelekea hufuzu kwa fainali la kombe la dunia litakalofanyika nchini Qatar 2022, michezo mbalimbali jana ilipigwa ulimwenguni kote kwa mataifa mbali mbali kusaka tiketi ya kufuzu michuano hiyo mikubwa ulimwenguni. Anaripoti Mintanga Hunda, TUDARCo…(endelea)

Kwa upanda wa barani Afrika ambayo inatoa timu tano kuwakilisha kwenye michuano hiyo, ilipigwa jumla ya michezo .. huku mingine ikitarajiwa kuendelea leo.

Katika michezo hiyo, Jamhuri ya kati ilikwenda sare ya 1-1, dhidi ya Cape Verde, Mali ikaibuka na ushindi wa bao 1-0, mbele ya Rwanda, huku Misri wakiwa nyumbani waliondoka na ushindi wa bao 1-0, dhidi ya Angola, Libya waliwaadhibu bao 2-0 Gabon.

Kwa upande wa timu ya taifa ya Senegal wao walitoka kifua mbele kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Togo na Guinea Bissau walilazimishwa sare ya bao 1-1 Wakiwa nyumbani dhidi ya Guinea.

Michezo mingine ya kusaka tiketi ya kufuzu fainali hizo, itapigwa hii leo kwa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), kushuka dimbani ugenini dhidi ya timu ya Taifa ya Congo kwenye mchezo wa kundi J.

Huku michezo mingine itazikutanisha Algeria dhidi ya Djibouti, Nigeria watamenyana na Burkinafaso, Kenya dhidi ya Uganda, Namibia kupepetena na Congo Brazaville, Morocco kuumana na Sudan na Madascar watakuwa nyumabani kuwakalibisha Benini.

error: Content is protected !!