May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mtibwa, Kagera hali tete ligi kuu

Spread the love

 

TIMU za Mtibwa na Kagera Sugar zimeendelea kujiweka katika mazingira magumu ya kusalia Ligi Kuu Tanzania Bara, baada ya kukubali kipigo katika michezo ya ligo hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mara … (endelea).

Ligi hiyo, imeendelea leo Jumatatu, tarehe 27 Aprili 2021, kwa michezo miwili kupigwa, Mtibwa waliwaalika Polisi Tanzania katika Uwanja wa Jamhuri, Morogoro huku Kagera, ikisafiri hadi Uwanja wa Karume, Mara kucheza na Biashara United.

Mtibwa imeendelea kusalia nafasi ya 14 kati ya timu 18 ikiwa na pointi 28, kati ya michezo 27, baada ya kukubali kipigo cha 2-1 kutoka kwa Polisi Tanzania. Ushindi huo wa Polisi, umewafanya kufikisha pointi 37 na kukwea hadi nafasi ya sita.

Ndugu zao, Kagera nao wamekubali kipigo kama hicho cha 2-1, dhidi ya Biashara. Ushindi huo wa Biashara umewafanya kufikisha pointi 44 na kusalia nafasi ya nne, kati ya michezo 28.

Kipigo cha Kagera inayofundishwa na Francis Baraza, aliyekuwa akiifundisha Biashara United, imeifanya kusalia nafasi ya 16 ya msimamo wa ligi kuu, ikiwa na pointi 27 kati ya michezo 28 iliyocheza.

Tangu kuanza kwa msimu wa 2020/21 wa Ligi Kuu, timu hizo za ‘walima miwa’ wa Morogoro na Kagera, zimekuwa hazina mwenendo mzuri.

error: Content is protected !!