September 23, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mtibwa, Coastal zabaki ligi kuu, Waziri Ummy…

Coastal Union

Spread the love

 

TIMU za Mtibwa Sugar ya Morogoro na Coastal Union ya Tanga zimefanikiwa kubaki Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa msimu ujao wa 2021/22. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Ni baada ya kupata matokeo mazuri katika michezo yao miwili iliyochezwa nyumbani na ugenini ya kuwania kubaki au kupanda kwenye ligi kuu.

Mtibwa ilikuwa inachuana na Transit Camp huku Coastal ikicheza na Pamba ya jijini Mwanza.

Leo Jumamosi, tarehe 24 Julai 2021, ilikuwa ni michezo ya marudiano ambapo Mtibwa imekubali kipigo cha 1-0 kutoka kwa Transit Camp katika uwanja wa Jamhuri Morogoro.

Hata hivyo, Mtibwa imesonga mbele kwani mchezo wa awali uliopigwa Uwanja wa Jamhuri, waliibuka na ushindi wa 4-1.

Huko Mkwakwani jijini Tanga, Coastal Union imefanikiwa kubaki baada ya kuifunga Pamba kwa 3-1 na katika mchezo wa awali uliochzwa Uwanja wa Nyamagana, Mwanza walifungana 2-2.

Awali leo Jumamosi asubuhi, Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi, Ummy Mwalimu alitembelea kambi ya Coastal na kuwaahidi wachezaji Sh.5 milioni endapo wataifunga Pamba na kubaki ligi kuu.

Ummy ambaye pia ni Mbunge wa Tanga Mjini (CCM), alilipia tiketi za mashabiki 1,000.

Mara baada ya kipenga cha mwisho, Waziri Ummy aliyekuwapo uwanja hapo akishangilia ushindi huo akizunguka uwanjani akishangilia kando ya mashabiki.

Hali ya usalama katika eneo la kuchezea ilibadilika baada ya mashabiki wa Coastal kuingia uwanjani kushangilia ushindi huo, jambo lililowafanya polisi kuanza kuwaondoa uwanjani.

Hata hivyo, kutokana na idadi kubwa ya mashabiki waliojazana katikati ya eneo la kuchezea, polisi wameshindwa kuwatoa.

Kocha wa Coastal, Juma Mgunda amesema ilikuwa ni mechi ngumu “sana na niliwaambia wachezaji kwani Pamba imekaa chini ya ligi kuu miaka 20. Huu umoja ambao umeonekana leo, uanzie chini kwani kwa umoja kama huu Coastal tusingecheza mtoana. Tunashukuru sana kwa ushirikiano.”

Naye Kocha wa Pamba, Ulimboka Mwakingwe amesema, “tunamshukuru Mungu kwa kumaliza mchezo salama, huu ndio mpira na nasikitika sana kwa uamuzi uliokuwa unafanywa na waamuzi, mpira umeonyeshwa kila mtu ameona ilivyo.”

error: Content is protected !!