September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mtia nia CCM Jimbo la Ubungo adakwa na Takukuru

African American in Prison

Spread the love

LIDA Lugani Mwakatuma, anayejipanga kugombea jimbo la Ubungo pamoja na viongozi watano wa Chama cha Mapinduzi (CCM), jimboni humo, wanashikiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), kwa tuhuma za rushwa na kuanza kampeni kabla ya muda. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Viongozi wanaoshikiliwa na TAKUKURU katika sakata hilo ni, Aisha Muki, Katibu Kata CCM kwenye Kata ya Mbezi, Subira Emmanuel, Katibu wa Umoja wa Wanawake CCM (UWT), Kata ya Mbezi na Athumani Yusuph Chuchu, Katibu Mwenezi CCM Kata ya Mbezi.

Charles Haule Denga, Mjumbe wa Kamati ya Siasa, Kata ya Mbezi na Angela Paul, Mjumbe wa Kamati ya Siasa Kata ya Mbezi.

Mwakatuma na wenzake wanatuhumiwa kuanza kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020, kabla ya wakati.

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumatatu tarehe 1 Juni 2020, na Pilly Mwakasege, Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa, Mwakatuma aliitisha kikao cha siri na wajumbe huo, ambacho kilifanyika kwa Katibu wa CCM Kata ya Mbezi, kwa lengo la kuwahonga ili wampigie kura ya uteuzi wa kugombea, kupitia chama hicho.

“Watuhumiwa hawa walikamatwa na maafisa wa TAKUKURU Wilaya ya Ubungo majira ya saa 3 usiku wa Mei 31, 2020. Wakiwa nyumbani kwa Katibu wa CCM Kata ya Mbezi wakifanya vikao vya siri na kupokea fedha za kutoka kwa mtia nia anayefanya kampeni ili wampigie kura muda utakapofika,” inaeleza taarifa ya Mwakasege.

Taarifa hiyo inadai kuwa, watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa kwenye harakati za kutoa na kupokea bahasha zenye fedha taslimu, za ushawishi kutoka kwa mtia nia, huku fedha hizo zikiwa tayari ndani ya bahasha.

“Kupitia operesheni hii, jumla ya bahasha tisa zilikamatwa na kila bahasha ilikuwa na Sh. 50,000, pia ndani ya mkoba wa mtia nia zilikutwa shilingi 240,000 ambazo zilikuwa kwenye mchakato wa kugawiwa kwa wajumbe hao, hivyo kufanya jumla ya Sh. 690,000,” inaeleza taarifa hiyo.

error: Content is protected !!