Monday , 5 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mteule wa JPM ajitetea: Sikuomba rushwa
Habari za Siasa

Mteule wa JPM ajitetea: Sikuomba rushwa

Spread the love

TUHUMA zilizoelekezwa kwa mteule wa Rais John Magufuli, Lengai Ole Sabaya, Mkuu wa Wilaya ya Hai (DC) kumwomba rushwa mfanyabiashara Curthebert Swai, limejibiwa. Anaandika Regina Mkonde…(endelea).

Mbele ya wanahabari tarehe 24 Julai 2019 DC Sabaya amesema, uamuzi wa Swai kudai kuombwa rushwa, unatokana na yeye (Sabaya) kumwondoa Swai katika eneo alilompora bibi mjane Mary Diriwa (86).

Amesema, eneo hilo alikuwa amelichukua hicho alimwondoa kwenye eneo hilo.

Swai anahoji, iweje sakata hilo litokee Novemba 2018, kisha aje kuliibua leo? “leo ndiyo unakuja kuchukua hatua uliyoombwa rushwa, baada ya kuchukua mali za hawa kina bibi?” amehoji.

Swai ambaye ni mmiliki wa Hoteli ya Kitalii ya Weruweru River Lodge, alirekodi kipande cha video akieleza namna Sabaya alivyomwomba rushwa ya Sh. 5 milion.

Alitoa tuhuma hizo katika mkutano wa kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mkoa wa Kilimanjaro kilichofanyika tarehe 22 Julai 2019.

Awali, mwandishi wa MwanaHALISI ONLINE, alimpigia simu Sabaya kutaka ufafanuzi kuhusu tuhuma hizo, alijibu kuwa anaandaa kikao na waandishi wa habari.

“Na ninyi waandishi wa habari mnanipigia simu kuniuliza juu ya hiyo ‘clip’ (kipande cha video), mkitaka maelezo yake chanzo chake ndiyo hiki,” alizungumza kwenye kikao hicho na wanahabari.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

Habari za SiasaTangulizi

Zanzibar watangaza rasmi kuwa shamba la Razaba ni mali yao

Spread the love  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imetangaza rasmi kwamba shamba...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Mwinyi azindua Kamati ya Maridhiano Visiwani

Spread the love  RAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk. Hussein...

error: Content is protected !!