Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mtemvu ahofia ‘kilichomwondoa’ Mnyika Kibamba
Habari za Siasa

Mtemvu ahofia ‘kilichomwondoa’ Mnyika Kibamba

Mbunge wa Kibamba, Issa Mtemvu
Spread the love

 

MBUNGE wa Kibamba, Issa Mtemvu ameonesha hofu yake ya kutoendelea kuwa mbunge wa jimbo hilo endapo changamoto ya upatikanaji wa maji haitatatuliwa kama ambavyo ilikuwa kwa mtangulizi wake John Mnyika. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Tatizo la upatikanaji wa maji katika jimbo la Kibamba limekuwa kero kubwa kwa muda mrefu na huwa inatajwa kuwa ndiyo sababu ya aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo kupitia Chadema, John Mnyika kutokubalika na kuondolewa katika uchaguzi wa mwaka 2020.

Mnyika alikuwa Mbunge wa Jimbo hilo tangu mwaka 2015 baada ya kugawanywa kutoka kwa lililokuwa jimbo la Ubungo.

Miongoni mwa malalamiko ya wananchi wa jimbo hilo ilikuwa ni Mnyika kutowatembelea wapiga kura wake na kusikiliza kero zao ikiwemo ya upatikanaji wa maji ili zipatiwe ufumbuzi.

Akizungumza leo Ijumaa tarehe 13 Mei 2022, Mtemvu amesema hakuna kiongozi anayeweza kwenda kwa wananchi wa jimbo hilo hivi sasa kwani ataishia kupigwa mawe kwa kutotekelezwa kwa ahadi walizotoa.

“Wananchi wa Kibamba wameendelea kulia na mimi nalia hapa kila siku, Kibamba wanalisha pugu, Kibamba wanalisha Ubungo lakini wananchi hawana maji katika jimbo la Kibamba,” amesema Mtemvu.

 

Aliyekuwa Mbunge wa Kibamba, John Mnyika

Amesema jimbo hilo linahitaji jicho la kipekee la Serikali kwani maeneo mengi hayana maji…“Naomba jicho la Serikali lijielekeze Kibamba vinginevyo mtamwondoa Mtemvu Kibamba,”

Ameyataja baadhi ya maeneo ambayo hayana maji kuwa ni Mpiji Magohe hakuna maji kabisa, Msumi, Msakuzi yote Kaskazini na Kusini, Kwembe, King’azi A “wanakunywa maji machafu.”

Mtemvu amesema jimbo hilo halina maji licha ya kuwa wapo viongozi wakubwa wa Serikali wakiwemo wabunge na mawaziri wanaishi humo na kusisitiza ipo siku atawataja.

Mbunge huyo amesema ipo miradi mitatu ukiwemo mradi wa Kitopeni, Mabwepande na tenki kutoka Kwembe- King’azi A haIjakamilika ya kukamilika tangu Desemba mwaka jana.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Deni la Serikali laongezeka kwa trilioni 11

Spread the loveDENI la Serikali imeongezeka kwa takribani Sh. 11 trilioni sawa...

Habari za SiasaKimataifa

Mwanaye rais jela miaka miaka 6 kwa dawa za kulevya

Spread the loveMwanawe rais wa zamani wa Guinea-Bissau amehukumiwa kifungo cha miaka...

Habari za SiasaTangulizi

Mapya yaibuka wamasai waliohamishwa Ngorongoro kwenda Msomera

Spread the loveMAPYA yameibuka kuhusu zoezi la Serikali kuwahamisha kwa hiari wamasai...

Habari za Siasa

Rais Samia ampongeza mpinzani aliyeshinda urais Senegal

Spread the loveRAIS wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, amempongeza mwanasiasa wa...

error: Content is protected !!