February 27, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mtemi Ramadhani ajiengua Uchaguzi Mkuu Simba

Spread the love

MGOMBEA wa nafasi ya Mwenyekiti kwenye Uchaguzi Mkuu wa klabu ya Simba, Mtemi Ramadhani amejondoa kwenye kinyang’anyiro hicho kwa sababu ya kuwa na majukumu yake binafsi yatakayoweza kumbana kwenye kutimiza wajibu wake kama kiongozi ndani ya klabu hiyo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu …  (endelea).

Katika mahojiano yake na moja ya kituo cha radio, Mtemi alithibitisha ni kweli ameshaandika barua kwenda kwenye kamati ya uchaguzi ya klabu hiyo kuomba jina lake lienguliwe katika mchakato huo ambao wanachama wanatarajaia kufanya maamuzi mwezi ujao.

“Ni kweli nimeandika barua kwenda kwa Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa klabu ya Simba kwamba naomba jina langu liondolewe kwenye kugombea nafasi ya mwenyekiti wa klabu ya Simba,” amesema Mtemi.

Aidha Mtemi aliongezea kuwa sababu iliyompelekea kuchukua maamuzi hayo ni kubanwa na majukumu yake binafsi yatajayopelekea kushindwa kutimiza majukumu yake kama akiwa kiongozi ndani ya klabu hiyo.

“Sababu kubwa sasa hivi nina majukumu mengi ninaweza kuhamia Dodoma kwa hiyo nadhani sitaweza kuitumikia vyema klabu yangu ya Simba lakini pia ningependa kuona klabu ina umoja katika kipindi hiki ambacho tunatarajia kutetea ubingwa wetu ambao tuliupata msimu uliopita,” alisema Mtemi.

Kujionmdoa kwa Mtemi katika Uchaguzi huo inamaanisha Sued Nkwabi anabaki peke yake katika nafasi hiyo ya uwenyekiti kwa sababu muda uliosalia hauruhusu mtu mwengine kuingia katika uchaguzi huo.

error: Content is protected !!