January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mtayachota kwa vidole vyenu

Spread the love

WA Kilindi juu. Mkampangia madumu Dadaangu wa Muyuni, anoizunguka nchi akimuombea ulaji mtaka mabadiliko kimtindo, Mapediloki. Eti nini, Magufuli si Ukawa? Anaandika Jabir Idrissa … (endelea).

Sijawahi kusikia wao wakisema mabadiliko, ni lugha ya Ukawa tangu 1992 walipokuwa Wanamageuzi kina mzee Ndim, sio Sisiem waloshindwa uongozi.

Kielelezo cha kushindwa miaka 54 ya uhuru Kilindi hawana maji safi na salama.

Inanirudisha Nzega, mkoani Tabora, nilikokwenda Aprili 2010 nikakuta nje tu ya mgodi wa Lusu ng’ombe wanakunywa maji machafu, ambayo kinamama walio kando na ndoo zao, waanasubiri zamu yao wachote.

Hii Tz ya ajabu. Ndo mana samtaimu rafki yangu wa K’ndoni Shamba ananiudhi kuwashabikia. Nimo kumzidi, na kule hakuna maendeleo zaidi ya mirungi na mafuriko kila msimu hata wa mvua kiduchu.

Nzega watu wanaishi mgodini panapochimbwa dhahabu nzuri kuliko zote Afrika, mpaka leo hawana maji. Niulizie kwa waziri wa maji nasikia anatetea kiti Mwanga, kwako wa nishati na madini unayetafuta Kibakwe, nawe Tamisemi uliyeko Mtwara Vijijini, yako wapi maji?

Sasa hii sirikali yao inadaiwa maji Lusu, Kilindi, Shinyanga kwenye ziwa Viktoria na kila kona nchini ikiwemo jijini Dsm. Madumu ya njano kila kipembe wanasaka maji kuuzia hohehahe. Wenye visima binafsi Mungu atawalipa, japo wengine wanauza ndoo kwa jero, sawa tu angalau yawepo.

Wang’ang’ania Ikulu wanachekesha kushindwa kote huko – washindwa kila nyanja ya maisha – wanazidi kulia mbele za wananchi, “Msituadhibu bado twafaa.”

Mbona mnatia adabu wenye nchi huku mkiwakejeli wapige mbizi Kigaa-na-mboni? Kweli wanafaa Sisiem, wapeni ridhaa muone raha.

Kilindi mtanyang’anywa madumu yenu yote na ndoo zote ili sasa maji mchote kwa vidole vyenu. Mmeambiwa sio, mchanganye na zenu.

Maji shida kila kona nchini miaka 54 ya uhuru; huku wakubwa wakifadhili mradi wa kutorosha Twiga, Faru na Chui wetu kimagendo. Waulizwe aliko Amrani, wakijibu nchinjwe!

Yale ya rafki yangu Bulembo potezea kama alivyopotezea babu Lubuva kuhusu kufujwa Tume kama ishaamua wao ndo wao hivo Oktoba 25 kutimiza ada tu; toba sikio, kila kitu kishapangwa!

Kumbe nisemeje kama malofa au hohehahe au watu wa Mathare au Mwaloni au Keko, Mbagala, Manzese na Tandale Uwanja wa Fisi tunaambiwa tuwapendao wasahau kungia sirikalini mana chama dume hawatafanyaga kosa la kuwapisha Ukawa jumba jeupe lile wapange. Huu si uhaini eti?

Hapana, ni kionjo tu cha kampeni; si braza Mbowe, mpambe wa Luwasa, nae kasema kura zitaibwa, yote sawa tu. Sivyo, mbona huyu mpambe yeye alionywa; na Luwasa akaonywa kwa kuwaomba Walutheri wamuombee ashinde? Usawa huoo? Ukawa vumilieni Mungu si Athumani.

Kama ‘urahisi’ ni kupiga pushapu na kurukaruka, sawa, mpeni mapediloki mtajua maana ya mvinyo uleule ndani ya chupa mpya.

Ila dogo wa Mvumi vituko, kasahau alivokataliwa na madenti wa kidato asiwe mgeni mhishimiwa katika mahafali ya sekondari ya jimboni. Madenti ‘visa vya wali wa maji’ kwelikweli, wakashikilia hakufika levo ile yao, asiende, hana cha kuwailimisha.

Sitaki maswali nshasema. Nipo huru sio!

error: Content is protected !!