August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mtatiro: Kambaya mimi sio ‘size’ yako

Julius Mtatiro, Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi CUF. Picha ndogo, Abdul Kambaya

Spread the love

JULIUS Mtatiro, Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi CUF, amesema hawezi kukutana na Abdul Kambaya, Naibu Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa CUF,  kujadili kuhusu mambo ya chama hicho, anaandika Hamisi Mguta.

Mtatiro ameyasema hayo leo baada ya Kambaya kumtaka wakutane na kujenga hoja kuhusu uhalali wa mambo uongozi na mambo yanayohusu mgawanyiko wa chama wakati akifanya mahojiano katika kipindi cha Power Breakfast cha Clouds kujadili kuhusu chama hicho.

Kambaya alituma ujumbe wa kutaka kukutana na Mtatiro kwa ajili ya mjadala baada ya kupiga simu na kuzungumza kwa muda mfupi wakati mazungumzo yakiendelea “Mimi mmenirekodi nimezungumza kidogo lakini mwenzangu anasikika na anajibu naomba tukutane siku mimi na yeye,” ulisomeka ujumbe huo.

Wakati ujumbe huo ukisomwa Mtatiro akakatika na kusema kuwa hawezi kuzungumza naye kwa sababu Kambaya ni aliyekuwa mwanachama.

“Mimi ni mwenyekiti ya kamati ya uongozi CUF, nimeteuliwa na baraza kuu la uongozi taifa, yeye ni mwanachama wa CUF aliyesimamishwa, hakuna uwiano, si kama namdharau tunatofautiana misimamo,” amesema Kambaya.

Amesema kuwa kama anataka kufanya mazungumzo katika chombo cha habari wapo wa saizi yake kama Mbarala Maharagande (Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano Taifa).

“Huwezi ukanileta mimi nije hapa kuzungumza na Abdul Kambaya, hatuwezi!! Tuna hadhi tofauti katika chama,” amesema.

error: Content is protected !!