April 12, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mtatiro atuliza polisi Tunduru

Spread the love

JULUS Mtatiro, Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, mkoani Ruvuma amelitaka Jeshi la Polisi wilayani humo kutotumia nguvu katika kushughulikia madereva wa pikipiki ‘Bodaboda’ wanaovunja sheria. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Mtatiro ametoa agizo hilo tarehe 7 Septemba 2019, katika mkutano wake na Jeshi la Polisi pia dereva wa Bodaboda. Ni baada ya polisi kuwapiga mabomu ya machozi Bodaboda kisha kuwakamata kwa nguvu Ijumaa iliyopita.

Katika mkutano huo, Mtatiro ameagiza jeshi hilo kuwaacha huru madereva waliokamatwa katika mkasa huo pamoja na pikipiki zao.

Pia, Mtatiro amepiga marufuku polisi kupiga madereva hao na kukimbizana nao pindi wanapofanya makosa bali wachukue namba zao za usajili.

“Polisi waache kuwapiga vijana wa bodaboda katika oparesheni za kipolisi, marufuku tabia ya polisi kukimbizana na bodaboda wachache watovu wa nidhamu na badala yake wachukue namba za pikipiki husika.

“Kisha kumuita mmiliki na dereva na kuwachukulia hatua za kisheria kwa sababu kufukuzana kumekuwa kukileta ajali mbaya,” ameagiza Mtatiro.

Aidha, Mtatiro amewataka vijana wa bodaboda kufuata sheria, ikiwa ni pamoja na pindi wasimamishwapo na polisi, wasimame na kutoa ushirikiano.

error: Content is protected !!