December 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mtanzania gaidi aliyejiua, alikuwa mgojwa wa akili

Kitanzi

Spread the love

RASHID Charles Mberesero, Mtanzania aliyehukumiwa kifungo cha maisha kutokana na kuhusika katika shambulio la kigaidi la Garisa, Kenya mwaka 2015, amejinyonga na kufariki dunia. Vinaripoti vyombo vya habari vya Kenya …. (endelea).

Kwa mujibu wa daktari wa magonjwa ya akili nchini humo, Mberesero alikuwa mgonjwa wa akili.

Taarifa inaeleza, Mberesero alijinyonga mwenyewe akiwa gerezani kwa kutumia blanketi lake alilokuwa akitumia kujifunika akiwa jela.

Daktari Mucheru Wang’ombe aliandika katika ripoti yake kwamba, Mberesero aliamini watu wote wa karibu naye walikuwa na imani za kishetani.

Mberesero alihukumiwa mwaka 2015 kwa kuhusika katika shambulio la kigaidi lililotokea katika Chuo Kikuu cha Garissa nchini Kenya na kusababisha watu 148 kufariki.

Katika shambulio hilo, wanne waliuawa kwa kupigwa risasi na wanajeshi wa Kenya chuoni hapo, lakini Rashid Charles, na wenzake wawili walikamatwa ambapo mwaka jana walihukumiwa kifungo cha maisha gerezani kwa kuhusika na ugaidi.

error: Content is protected !!