April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mtanzania awa Mwafrika wa kwanza kutwaa tuzo ya Brady

Joyce Singano

Spread the love

 

JOYCE Singano, mwanasayansi na mtafiti, amekuwa Mwafrika wa kwanza kutwaa tuzo maarufu inayotolewa kwa wataalamu wa maiamba duniani ‘Brady Meda.’ Inaripoti mitandao ya kimataifa … (endelea).

Brady Medal ndio tuzo kubwa zaidi duniani inayotolewa kwa watafiti waliofanya vizuri kwa mwaka husika. Singano ameibuka kinara wa utafiti kwa mwaka 2020.

Singano mwenye mchango mkubwa katika Shirika la Maenedeleo la Petroli Tanzania (TPDC),ametwaa tuzo hiyo kubwa zaidi miongoni mwa tuzo zinazotolewa kwa watafiti wa ukadiriaji wa miamba wanaotumia visukuku viumbe ambao wanapatikana ardhini.

“…ni kwamba kwa mwaka ule wa 2020, walikuja na wenzako wote wakatathminiwa, wewe ukaonekana unastahili kupata tuzo hiyo.

“Kwangu mimi ni heshima kubwa mno ambayo sikuitegemea kabisa, na hasa ukitazama research (tafiti) wanazotazama hivi karibuni, hawatazami research ya mwaka mmoja na hawatazami faida ya mtu mmoja mmoja, wanatanzama je umesaidia watu wangapi katika hiyo research yako na dunia imefaidikaje?” ameeleza Singano ambaye ni mstaafu kwa miaka 10 sasa.

Amesema, alidokezwa kwamba ushindi wake unatokana na kazi alizowahi kufnya tangu mwaka 1999 mpaka 2009, na kwamba zimeonekana kuwa na mchango mkubwa kwa watu wengi walipitia kwake.

‘Brady Medal’ ni nini?

Hii ndio tuzo ya juu zaidi ya Jumuiya ya Wanasaansi watafiti (Micropalaeontological). Imeanzishwa kwa heshima ya wanasayansi watafiti George Stewardson Brady (1832-1921) na Henry Bowman Brady (1835-1891) kwa kutambua mchango wao kwenye utafiti kupitia viumbe asili.

Medali hiyo hutoleewa kwa wanasayansi ambao wamekuwa na ushawishi mkubwa kupitia tafiti zao. Huduma kwa jamii ya kisayansi pia huwa sehemu ya sababu ya kuzingatiwa na kamati ya tuzo hiyo.

error: Content is protected !!